Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mafuriko Libya: 'Nimepoteza takriban wanafamilia 50'

Mafuriko Libya: 'Nimepoteza Takriban Wanafamilia 50' Mafuriko Libya: 'Nimepoteza takriban wanafamilia 50'

Thu, 14 Sep 2023 Chanzo: Bbc

Walibya wamekuwa wakizungumza kuhusu kupoteza familia nzima kutokana na mafuriko mabaya yaliyotokea nchini humo.

Usama Al Husadi, dereva mwenye umri wa miaka 52 ambaye alikuwa akifanya kazi usiku wakati maafa yalipotokea, hakuweza kumpata mke wake na watoto watano baada ya kupekua kila mahali.

Simu ya mkewe imezimwa.

Huku akilia, aliliambia shirika la habari la Reuters kuwa amepoteza "takriban watu 50 kutoka kwa familia ya baba yangu... ambao hawajulikani walipo na waliofariki".

Wali Eddin Mohamed, mfanyakazi wa kiwanda cha matofali mwenye umri wa miaka 24, amepoteza wanafamilia 15 na marafiki tisa.

"Wote walisombwa na bonde hadi baharini," aliambia Reuters.

"Mungu awarehemu na awape pepo."

Chanzo: Bbc