Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mafuriko Kenya: Serikali yaamuru kuhamishwa kwa watu

Mafuriko Kenya: Serikali Yaamuru Kuhamishwa Kwa Watu Mafuriko Kenya: Serikali yaamuru kuhamishwa kwa watu

Fri, 3 May 2024 Chanzo: Bbc

Serikali ya Kenya imewaamuru watu wanaoishi karibu na mabwawa na hifadhi 178 kuhama huku mvua kubwa ikiendelea kunyesha.

Wizara ya mambo ya ndani ilionya kwamba vyanzo vya maji "vimejaa au karibu kujaa na vinaweza kumwagika wakati wowote, na kusababisha hatari kubwa kwa watu wanaoishi maeneo jirani.

Imewapa wakazi wanaoishi karibu na maeneo hayo - pamoja na wale walio ndani ya ukanda wa ardhi yenye unyevu wa mita 30 (98ft) wa Mto Nairobi - saa 24 kutoka 18:30 saa za ndani siku ya Alhamisi kuondoka.

Mvua kubwa za hivi majuzi zimesababisha mafuriko makubwa na maporomoko ya ardhi kote Kenya na Tanzania.

Takriban watu 188 wamefariki nchini Kenya tangu Machi, huku wengine 90 wakitoweka, kulingana na makadirio rasmi ya hivi punde.

Watu wengine 155 wamefariki nchini Tanzania.

Takriban watu 50 wanadhaniwa kufa wakati maporomoko ya udongo yalipokumba vijiji vya Kenya karibu na Mai Mahiu walipokuwa wamelala. Mafuriko pia yameathiri mji mkuu, Nairobi.

Maafisa wanatarajia hali kuwa mbaya zaidi katika siku zijazo na kuwasili kwa hali mbaya ya hewa.

"Kikubwa zaidi, eneo la pwani huenda likakumbwa na Kimbunga Hidaya, ambacho kitasababisha mvua kubwa, mawimbi makubwa na upepo mkali ambao unaweza kuathiri shughuli za baharini katika Bahari ya Hindi," ofisi ya Rais wa Kenya William Ruto ilisema.

Idara ya hali ya hewa nchini Kenya ilisema Nairobi inatarajiwa kuwa miongoni mwa maeneo yaliyoathiriwa zaidi na dhoruba hiyo.

Wizara ya mambo ya ndani ilisema hali "inaweza kuwa mbaya kwa sababu udongo kote nchini umejaa maji kikamilifu"

Chanzo: Bbc