Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mafuriko DRC: Idadi ya waliofariki yafikia 176

Mafuriko DRC: Idadi Ya Waliofariki Yafikia 176 Mafuriko DRC: Idadi ya waliofariki yafikia 176

Sat, 6 May 2023 Chanzo: Bbc

Mamlaka mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo zinasema idadi ya watu watu wanaosadikiwa kufa kutokana na mafuriko na maporomoko ya udongo imeongezeka na kufikia 176.

Gavana wa jimbo la Kivu Kusini anasema watu zaidi bado hawajulikani walipo, wanahofiwa kufukiwa chini ya udongo.

Vijiji vya Bushushu na Nyamukubi - vilisombwa na maji baada ya mito ya mashariki mwa Congo kuvunja kingo zake.

Pia kumeripotiwa maporomoko makubwa ya udongo ambayo yaliharibu nyumba zilizojengwa kwa mbao na paa za bati.

Vyombo vya habari vya ndani vinaripoti kwamba katika moja ya vijiji zaidi ya robo tatu ya nyumba zote zimesombwa na maji ikiw ani pamoja na vituo vya afya na shule.

Upande wa pili wa Ziwa Kivu katika nchi jirani ya Rwanda takriban watu mia moja na thelathini walikufa kutokana na mafuriko na maporomoko ya udongo.

Chanzo: Bbc