Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mafuriko DR Congo: 'Watu bado wanahitaji msaada'

Mafuriko DR Congo: 'Watu Bado Wanahitaji Msaada' Mafuriko DR Congo: 'Watu bado wanahitaji msaada'

Tue, 9 May 2023 Chanzo: Bbc

Watu walioathiriwa na mafuriko na maporomoko ya ardhi katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DR Congo) "bado wanahitaji sana" usaidizi wa kibinadamu, mtaalamu wa mipango kutoka shirika la misaada la Corus International ameambia kipindi cha Newsday cha BBC.

Siku ya Jumatatu mamlaka ilitangaza kuwa idadi ya vifo imefikia zaidi ya 400, na idadi hiyo inatarajiwa kuongezeka Jean Claude Nzay alisema.

"Tunazungumza kuhusu watu ambao wamepoteza kila kitu", Bw Nazy alisema, akiongeza kuwa watu wameumizwa sana na "hawawezi hata kulia".

Mafuriko na maporomoko ya ardhi yalikumba vijiji viwili mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wiki iliyopita, na tangu wakati huo watu wamekuwa wakichimba tope kwa mikono katika msako mkali wa kuwatafuta jamaa waliopotea.

Bw Nzay aliongeza kuwa mamlaka zinahitaji kuanzisha vituo vya kisaikolojia ambapo watu wanaweza kuzungumza waziwazi kuhusu huzuni yao.

Chanzo: Bbc