Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mafao ya Kenyatta kupigiwa kura Bungeni

Uhuru Kenyatta Bilionaire Mafao ya Kenyatta kupigiwa kura Bungeni

Thu, 4 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Bunge la Kitaifa la Kenya linahitaji kura za walio wengi kusitisha mafao ya kila mwezi na marupurupu mengine ambayo Rais wa zamani wa Kenya, Uhuru Kenyatta anapata kwa kinachoelezwa kuwa anajihusisha na siasa baada ya kustaafu.

Mbunge wa Gatundu Kusini, Gabriel Kagombe amewasilisha hoja katika Bunge la Kitaifa Jumanne Mei 2, 2023 akitaka Kenyatta anyimwe marupurupu yake ya kustaafu.

Hoja hiyo pia inalenga kusitisha mafao na marupurupu mengine ya aliyekuwa Waziri Mkuu, Raila Odinga na aliyekuwa Makamu wa Rais, Kalonzo Musyoka.

Hoja hiyo inaungwa mkono kwa kiasi kikubwa na wabunge wanaounga mkono Muungano wa Kenya Kwanza wa Rais William Ruto.

Uamuzi wa kusitisha mafao ya Odinga na Musyoka utaamuliwa na si chini ya nusu ya wabunge, kwa mujibu wa Sheria ya Mafao ya Kustaafu (Naibu Rais na Maofisa Walioteuliwa).

Kagombe pia anataka Hazina ya Taifa kurejesha angalau Sh844 milioni ambazo zimelipwa kwa maofisa watatu wa zamani baada ya kuondoka ofisini.

Mbunge huyo wa awamu ya kwanza anawatuhumu watatu hao kwa kujihusisha na siasa kali huku wakiendelea kupokea mafao yao ya kustaafu, jambo ambalo anasema ni kinyume na vifungu vya Sheria ya Mafao ya Kustaafu ya Rais ya mwaka 2003 na Sheria ya Mafao ya Kustaafu (Naibu Rais na Maofisa Wateule) ya mwaka 2015.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live