Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Maelfu ya watoto wanyimwa elimu Cameroon kwa kukosa yeti vya kuzaliwa

Maelfu Ya Watoto Wanyimwa Elimu Cameroon Kwa Kukosa Yeti Vya Kuzaliwa.jpeg Maelfu ya watoto wanyimwa elimu Cameroon kwa kukosa yeti vya kuzaliwa

Sat, 17 Jun 2023 Chanzo: Voa

Dunia inapoadhimisha Siku ya Kimataifa ya Mtoto wa Afrika tarehe 16 Juni, makundi ya haki za binadamu na maafisa nchini Cameroon wamesambaza vyeti vya kuzaliwa kwa watoto 30,000 miongoni mwa watoto milioni kadhaa walionyimwa elimu kwa kutokuwa na hati hiyo.

Idadi kubwa ya watoto ambao hawakuwa na vyeti vya kuzaliwa wanatoka katika mikoa ya magharibi na katika mpaka ulioko kaskazini mwa Cameroon na Nigeria ambako kuna mizozo ya wanaotaka kujitenga na kundi la Boko Haram ambalo limewakosesha makazi mamilioni ya watu.

Serikali ya Cameroon imesema wiki hii maelfu ya watoto wamefika katika mabaraza mbalimbali ya wilaya nchini kuchukua vyeti vyao vya kuzaliwa.

Miongoni mwa watoto wanaotarajia kutengenezewa vyeti vyao vya kuzaliwa na Halmashauri ya Jiji la Youande ni Mustapha Issa mwenye umri wa miaka 17.

Mustapha alisema yeye ni miongoni mwa maelfu kadhaa ya watoto walionyimwa elimu kwa kutokuwa na vyeti vya kuzaliwa.

Mustapha alisema alikwenda katika Halmashauri ya jiji la Yaounde siku ya Alhamisi na kumsihi meya wa jiji hilo ili amsaidie yeye na watoto wengine ambao hawakuweza kupata elimu kwa sababu hawakuwa na vyeti vya kuzaliwa.

Alisema baadhi ya akina mama wa baadhi ya watoto hao wanaotamani kupata elimu, walijifungulia nyumbani na hivyo kushindwa kuwaandikisha.

Wizara ya elimu ya sekondari ya Cameroon ilisema ni lazima kwa watoto kuwasilisha vyeti vyao vya kuzaliwa kabla ya kuendelea na masomo yao baada ya kumaliza elimu ya msingi.

Mustapha alisema walioacha shule wanakuwa watoto wa mitaani, waraibu wa dawa za kulevya na kuingia katika magenge ya uhalifu.

Serikali ya Cameroon ilisema maelfu ya vyeti vya kuzaliwa vilipotea au kuharibiwa katika mzozo wa kutaka kujitenga wa Cameroon ambao hadi sasa umewakosesha makazi watu 750,000 katika mikoa ya magharibi inayozungumza lugha ya Kiingereza, wengi wao wakiwa wanawake na watoto

Chanzo: Voa