Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Maelfu ya wanawake Afrika kupoteza maisha Uingereza kupunguza misaada: Ripoti

Maelfu Ya Wanawake Afrika Kupoteza Maisha Uingereza Kupunguza Misaada: Ripoti Maelfu ya wanawake Afrika kupoteza maisha Uingereza kupunguza misaada: Ripoti

Wed, 2 Aug 2023 Chanzo: Bbc

Maelfu ya wanawake barani Afrika watapoteza maisha wakiwa wajawazito na wengine wakati wa kujifungua kutokana na kupunguzwa kwa bajeti ya misaada ya Uingereza inayokwenda nje ya nchi, mawaziri wameonywa.

Kwa mujibu wa tathmini ya ndani ya watumishi wa umma, karibu wanawake 200,000 zaidi pia watakabiliwa na utoaji mimba usio salama.

Ripoti yao inaonyesha athari za kupunguzwa kwa bajeti ya misaada ya nje mwaka huu. Hata hivyo Ofisi ya Mambo ya Nje inasema bajeti yake kwa nchi za kipato cha chini imepunguzwa kwa musa tu ili kufikia lengo la kuweka akiba, lakini itapanda na kukaribia mara mbili.

Waraka wa ndani unasema kupunguzwa kwa misaada kwa 76% kwa Afghanistan kutaacha baadhi ya wanawake na wasichana walio hatarini zaidi duniani bila huduma muhimu. Na nusu milioni ya wanawake na watoto nchini Yemen hawatapata huduma za afya.

Bajeti ya Idara ya Usaidizi wa Maendeleo ya Nje ina thamani ya zaidi ya £900m kwa mwaka huu. Hitimisho hilo linakuja katika tathmini iliyofanywa na watumishi wa umma wa Ofisi ya Mambo ya Nje mapema mwaka huu, ili kuwafahamisha mawaziri kabla hawajaamua cha kupunguza.

Chanzo: Bbc