Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Maelfu ya walinda amani wa AU wauawa Somalia

Maelfu Ya Walinda Amani Wa AU Wadaiwa Kufa Kwenye Operesheni Ya Somalia Maelfu ya walinda amani wa AU wadaiwa kufa kwenye operesheni ya Somalia

Wed, 12 Apr 2023 Chanzo: Voa

Mkuu wa ujumbe wa walinda amani wa Umoja wa Afrika ameambia VOA kwamba maelfu ya walinda usalama wa AU wameuawa huku mamia wakijeruhiwa nchini Somalia tangu walipoingia nchini huko, mnamo mwaka wa 2007.

Wanajeshi hao walipelekwa nchini humo ili kulinda serikali, pamoja na maeneo mengine muhimu dhidi ya mashambulizi ya kundi la kigaidi la al Shabab linalohusishwa na al Qaida.

Mohamed El Amine Souef ambaye ni mjumbe mwakilishi maalum wa mwenyekiti wa tume ya Umoja wa Afrika nchini Somalia amefichua hayo wakati wa mahojiano kupitia kipindi cha uchunguzi cha VOA Idhaa ya kisomali.

Souef alisema kwamba vikosi hivyo havikuwa vimeandaliwa vilivyo wakati kukiwa hakuna afisi za kiutawala kwenye mji mkuu wa Mogadishu. Ameongeza kusema kwamba kesi nyingi kuhusu vikosi hivyo hazijaorodheshwa vilivyo.

Kikosi hicho mwanzoni kilijulikana kama African Union Mission in Somalia, na mara ya kwanza kilitumwa Mogadishu Machi 2007, kikijumuisha wanajeshi wa Uganda. Aprili 2022, jina la kikosi hicho lilibadilishwa na kuwa African Union Transition Mission au ATMIS, kikiwa na nia ya kuondoka nchini humo kufikia Desemba mwaka ujao baada ya wanajeshi wa Somalia kuchukua jukumu la kulinda nchi.

ATMIS sasa hivi kina takriban walinda amani 19,000 nchini humo. Tangu wakati huo, wanajeshi walioorodheshwa kufa ni takriban 4,000. Kwa mujibu wa maafisa waliowahi kuhudumu kwenye kikosi hicho, idadi ya waliokufa wakiwemo waliolemazwa huenda ikafikia 5,000.

Chanzo: Voa