Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Maelfu ya Wakenya wamekwama Lebanon

LEBANON KENYA Maelfu ya Wakenya wamekwama Lebanon

Tue, 1 Oct 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Maelfu ya Wakenya wamekwama nchini Lebanon huku utawala wa Kizayuni wa Israel ukiendeleza mashambulizi yake ya kigaidi dhidi ya nchi hiyo ya Kiarabu.

Kwa mujibu wa gazeti la The East African, siku ya Alhamisi serikali ya Kenya ilisema Wakenya walioko Lebanon wako salama bila kutoa taarifa kuhusu iwapo kuna mpango wa kuwaondoa katika nchi hiyo.

Halima Mohammud, balozi wa Kenya nchini Lebanon, mwenye makao yake nchini Kuwait, ameliambia gazeti hilo kwamba ubalozi wake umewasiliana na Wakenya walioko Lebanon na wamepata taarifa za sehemu ya kupiga simu iwapo watataka msaada. Aidha amesema hakuna Mkenya aliyeuawa au kujeruhiwa wakati huu wa kushadidi mashambulizi ya Israel dhidi ya nchi hiyo.

Kwa mujibu wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Kenya, kuna Wakenya wasiopungua 26,599 wanaoishi nchini Lebanon.

Jeshi la kigaidi la Israel lilianzisha mashambulizi ya kikatili dhidi ya Lebanon kuanzia Jumatatu ya wiki iliyopita ambapo limewaua mamia ya watu wa Lebanon, wakiwemo wanawake na watoto.

Sayyid Hassan Nasrullah, Kiongozi wa muda mrefu wa Hizbullah, aliuawa katika shambulio la kigaidi la anga lililofanywa na jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel kusini mwa Beirut siku ya Ijumaa kwa kutumia mabomu mazito uliopatiwa utawala huo haramu na Marekani.

Katika kujibu jinai za kigaidi za Israel, Harakati ya Hizbullah ya Lebanon imevurumisha makombora ya Fadi-1 dhidi ya kambi za jeshi la Israel katika maeneo ya kaskazini yanayokaliwa kwa mabavu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live