Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Maelfu waokolewa Msumbiji, wengine walijificha Hotelini

Screenshot 2021 03 29 At 02.14.10 660x400.png Maelfu waokolewa Msumbiji, wengine walijificha Hotelini

Tue, 30 Mar 2021 Chanzo: millardayo.com

Mashirika ya misaada ya kiutu na ya haki za Binadamu yamesema maelfu ya Watu Manusura wa shambulizi la kigaidi kwenye Mji wa Palma, Jimboni Cabo Delgado Msumbiji wameokolewa jana.

Jumatano iliyopita Wanamgambo wenye itikadi kali walianza kufanya mashambulizi katika mji huo wenye hazina ya gesi na kulazimisha Watu 200 wakiwemo wa Wafanyakazi wa kigeni wa kampuni ya gesi kukimbilia kwenye Hoteli na kukaa zaidi ya siku tatu kabla ya kuokolewa.

Tangu Oktoba 2017 Wapiganaji wenye itikadi kali wamevizingira Vijiji na Miji katika maeneo mbalimbali ya Kaskazini mwa Msumbiji na kusababisha karibu Watu 700,000 kuyakimbia makazi yao. 

ULIPITWA? TAZAMA HAPA LIVE RAIS SAMIA SULUHU AKITANGAZA KUMSIMAMISHA KAZI MKURUGENZI MKUU WA MAMLAKA YA BANDARI NA MENGINE.

Chanzo: millardayo.com