Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Maelfu wanatoroka mauaji mapya ya kikabila huko Darfur nchini Sudan

Maelfu Wanatoroka Mauaji Mapya Ya Kikabila Huko Darfur Nchini Sudan Maelfu wanatoroka mauaji mapya ya kikabila huko Darfur nchini Sudan

Wed, 8 Nov 2023 Chanzo: Bbc

Kumekuwa na ongezeko kubwa la idadi ya watu wanaotoroka ghasia mpya katika eneo la Darfur nchini Sudan, shirika la usaidizi la matibabu linasema.

Mashuhuda wameshutumu vikosi vya Rapid Support Forces washirika wake kwa kutekeleza mauaji ya kikabila dhidi ya watu wasio Waarabu huko Darfur Magharibi.

RSF haikutoa maoni yake mara moja kuhusu madai hayo lakini awali ilisema haikuhusika katika kile ilichokitaja kuwa "mgogoro wa kikabila".

Watu elfu saba wamevuka mpaka wa Sudan na kuingia Chad katika muda wa siku tatu, Médecins Sans Frontieres (MSF) inasema.

Miongoni mwao ni makumi ya watu waliojeruhiwa. MSF inasema wakimbizi hao ni hasa wanawake na watoto ambao wanatoroka ghasia bila chochote.

Shirika la habari la Reuters linaripoti msururu wa wanaume wamevuka kutoka Darfur kwenda Chad huko Adre, yapata kilomita 27 (maili 17) magharibi mwa mji mkuu wa jimbo, El Geneina.

Baadhi wamewaambia waandishi wa habari kuhusu ukatili unaofanywa katika maeneo ya Darfur Magharibi ambayo yametekwa na RSF.

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi linasema mgogoro wa kibinadamu "usiofikirika" unaendelea nchini Sudan.

Takriban watu milioni sita wamekimbia makazi yao tangu vita kati ya jeshi la Sudan na RSF kuanza katikati ya mwezi Aprili.

Zaidi ya watu 500,000 wamevuka na kuingia Chad, wengi wao kutoka Darfur Magharibi, Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM) linasema.

Vikosi hasimu havijapiga hatua kuelekea kusitisha mapigano katika mazungumzo yao ya hivi punde, badala yake walikubali kuwezesha uwasilishaji wa misaada, mwenyeji wa Saudi Arabia alisema Jumanne.

Chanzo: Bbc