Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Maelfu wakwama katika mafuriko ya Somalia - UN

Maelfu Wakwama Katika Mafuriko Ya Somalia   UN Maelfu wakwama katika mafuriko ya Somalia - UN

Mon, 6 Nov 2023 Chanzo: Bbc

Maelfu ya watu wamekwama katika maeneo yaliyofurika kufuatia mvua kubwa iliyonyesha katika jimbo la Jubbaland nchini Somalia, shirika la Umoja wa Mataifa la misaada ya kibinadamu linasema.

Mvua kubwa iliyonyesha mwezi uliopita imeongeza kiwango cha maji kwenye mto Juba, na kusababisha mafuriko katika maeneo ya mito ya jimbo hilo, Ofisi ya Uratibu wa Masuala ya Kibinadamu (Ocha) ilisema katika taarifa yake.

"Katika wilaya ya Luuq, watu 2,400 wamenaswa katika eneo lililozingirwa na maji," iliongeza taarifa hiyo.

Juhudi za mamlaka na washirika wa uokoaji zinaendelea kuwaondoa wenyeji waliokwama.

Takriban watu 14 wamefariki na 47,000 wamekimbia makazi yao kutokana na mafuriko yaliyotokea nchini Somalia tangu mwezi uliopita, Ocha ilisema katika taarifa yake ya awali.

Waziri wa Habari wa Somalia Daud Aweis alisema mafuriko hayo, ambayo pia yaliathiri Hirshabelle na majimbo ya kusini magharibi, yamesababisha uharibifu mkubwa.Aliomba uungwaji mkono, akiongeza kuwa hali ni mbaya.

Nchi inakumbwa na mvua kubwa kuliko kawaida baada ya kuibuka kutokana na ukame mbaya zaidi katika miongo minne.

Shirika la Chakula na Kilimo limeonya juu ya hatari kubwa ya mafuriko, haswa katika eneo la kusini-magharibi la Gedo.

Chanzo: Bbc