Idadi ya watu wanaokimbia machafuko katika jimbo la Darfur huko Sudan inaripotiwa kuongezeka kufuatia wimbi jipya la mauaji ya kikabila.
Taarifa zaidi zinasema, kumekuwa na ongezeko kubwa la idadi ya watu wanaotoroka ghasia mpya katika eneo la Darfur nchini Sudan, shirika la usaidizi la matibabu linasema.
Mashuhuda wameshutumu vikosi vya Rapid Support Forces washirika wake kwa kutekeleza mauaji ya kikabila dhidi ya watu wasio Waarabu huko Darfur Magharibi.
RSF haikutoa maoni yake mara moja kuhusu madai hayo lakini awali ilisema haikuhusika katika kile ilichokitaja kuwa "mgogoro wa kikabila".
Watu wanaokimbilia Chad kutoka Sudan, wameelezea juu ya ongezeko jipya la mauaji ya kikabila katika jimbo la Darfur Magharibi, wanamgambo wa RSF walipoiteka kambi kuu ya jeshi katika mji mkuu wa jimbo hilo, El Geneina. Wanamgambo wa RSF wamekuwa wakipambana na jeshi rasmi tangu Aprili mwaka huu katika mzozo ambao umewalazimisha wakaazi wengi wa Darfur kuyahama makazi yao. Wapiganaji wa Kikosi cha Usaidizi wa Haraka (RSF)
Wakati huo huo, Saudi Arabia imetangaza kuwa, pande zinazohasimiana nchini Sudan hazijapiga hatua yoyote kuelekea kufikia makubaliano ya usitishwaji wa mapigano katika mazungumzo yao ya sasa.
Shirika rasmi la habari la Saudi Arabia limeripoti kwamba mwenyeji wa mazungumzo hayo, Saudi Arabia inasikitika kwamba pande hizo mbili zimeshindwa kuafikiana kuhusu mkataba wa kusitisha mapigano wakati wa duru hii ya kwanza, kwa kuwa hakuna suluhisho la kijeshi linalokubalika kwa mzozo wa Sudan