Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Maelfu wakamatwa Brazil kwa kuvamia Ikulu na Bunge

Maelfu Wakamatwa Brazil Kwa Kuvamia Ikulu Na Bunge Maelfu wakamatwa Brazil kwa kuvamia Ikulu na Bunge

Tue, 10 Jan 2023 Chanzo: bbc

Takriban watu 1,500 wamekamatwa nchini Brazil baada ya wafuasi wa aliyekuwa rais wa nchi hiyo Jair Bolsonaro kuvamia majengo ya serikali ikiwemo bunge, Ikulu ya rais na Mahakama ya Juu katika mji mkuu Brasília.

Ghasia hizo zilikuja wiki moja baada ya Rais Luiz Inácio Lula da Silva kuapishwa kuwa rais wa nchi hiyo. Baada ya kuapishwa alishutumu "vitendo vya kigaidi" na kuapa kuwaadhibu wahusika.

Bwana Bolsonaro hajakubali kushindwa katika uchaguzi uliokuwa na upinzani mkali wa Oktoba mwaka jana ambao uliligawanya taifa hilo, na alisafiri kwa ndege hadi Marekani kabla ya makabidhiano ya madaraka Januari 1.

Siku ya Jumatatu, alilazwa hospitalini huko Florida akiwa na maumivu ya tumbo.

Makumi kwa maelfu ya watu sasa wanaandamana katika jiji kubwa zaidi la Brazili São Paulo kupinga matokeo na kuunga mkono maadili ya kidemokrasia.

Chanzo: bbc