Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Maelfu waandamana nchini Morocco kupinga uhusiano na Israel

Maelfu Waandamana Nchini Morocco Kupinga Uhusiano Na Israel Maelfu waandamana nchini Morocco kupinga uhusiano na Israel

Mon, 12 Feb 2024 Chanzo: Bbc

Maelfu ya raia wa Morocco wameandamana katika mitaa ya Rabat wakitaka kusitishwa uhusiano na Israel, kutokana na hatua zake huko Gaza.

Baadhi walipeperusha mabango wakisema "komesha mauaji" na "ukawaida ni uhaini" wakati wa maandamano ya Jumapili.

Wanasiasa kutoka nyanja mbali mbali wanaripotiwa kuwa miongoni mwa waandamanaji hao.

Morocco ilianzisha uhusiano wa kidiplomasia na Israel mwaka 2020 chini ya Mkataba wa Abraham uliosimamiwa na Marekani.

Kama sehemu ya mpango huo, Rabat ilipokea utambuzi wa Washington wa madai yake ya uhuru juu ya eneo linalozozaniwa la Sahara Magharibi.

Upinzani dhidi ya makubaliano hayo umekua kwa kasi tangu kuanza kwa vita huko Gaza.

Chanzo: Bbc