Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Maelfu waandamana kupinga machafuko

Saga Maelfu waandamana kupinga machafuko

Thu, 16 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Maelfu ya raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), wameandamana katika mitaa ya mji mkuu wa Goma uliopo jimbo la Kivu Kaskazini, kupinga kitendo cha nchi ya Rwanda kuwaunga mkono waasi wa kikundi cha wapiganaji wa M23.

“Rwanda inatushambulia kwa miaka 20 sasa, leo tunaomba umakini wa watu, leo tunasimama sote kutetea Taifa na tuko nyuma ya FARDC, jeshi letu linalopigana kuwaondoa adui. Rwanda inatushambulia na leo tunamwambia Kagame aache kucheza na Wakongo”, alionya Chance Makale aliyeshiriki maandamano hayo.

Mwandamanaji wa kike, Polyn Nadège amesema “Serikali yetu lazima ijue kuwa jeshi la Kongo lina mamluki ndani yake na mamluki hawa wageni lazima wafukuzwe na ikiwa wataakifanikiwa, basi DRC itakuwa na nguvu ya kuwapiga hawa askari wa Rwanda wanaotuletea mateso makubwa.”

Naye Fiston Ketha akaongeza kuwa “kwa sasa nchi yetu inavamiwa na nchi jirani na hatutakubali machafuko haya makubwa ambayo yamedumu kwa miaka mingi katika nchi yetu na tumekusanyika hapa leo ili kuonyesha kuliungaji mkono jeshi letu.”

Waasi hao, walianza mapigano mapya Novemba 2021, baada ya kuishutumu serikali ya Kinshasa kwa kushindwa kuheshimu makubaliano ya mwaka 2009 ya kuwajumuisha wapiganaji wake ndani ya Jeshi na Juni 13, 2022 waasi hao waliteka mji wa kibiashara wa Bunagana.

Maandamano hayo yanafanyika ikiwa imepita siku moja baada ya serikali ya DRC kusisitiza kuwa Rwanda inaunga mkono kundi la waasi la M23, tuhuma ambazo zinakanushwa na Serikali ya Rais Paul Kagame.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live