Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Maelfu waandamana Morocco kupinga uhusiano na Israel

Israel Morocco Waandamana Tena Maelfu waandamana Morocco kupinga uhusiano na Israel

Mon, 27 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Makumi ya maelfu ya raia wa Morocco waliandamana katika miji ya kaskazini-magharibi ya Tangier na Casablanca siku ya Jumapili kuunga mkono Wapalestina, huku wakitilia mkazo hasa hali ya Gaza, eneo ambalo linakabiliwa na maafa makubwa kufuatia mashambulizi ya mabomu ya jeshi katili la Israel.

Washiriki wa maandamano ya Tangier wamepeperusha bendera za Palestina na Morocco, pamoja na picha za msikiti wa Al-Aqsa na wahasiriwa wa mashambulizi ya Israel huko Gaza.

Maandamano hayo, ambayo yaliungwa mkono na mashirika kadhaa ya kiraia, ikiwa ni pamoja na Harakati ya Morocco ya Kuunga Mkono Palestina na Kupinga Uhusiano na Israel na Mamlaka ya Morocco ya Kuunga mkono Malengo ya Kitaifa, yameangazia harakati za Kiislamu za ukombozi (muqawama), ambazo zimekuwa muhimu katika kuachiliwa huru wanawake wa Kipalestina waliokuwa wakishikiliwa katika jela za Israel.

Washiriki pia wametaka ofisi ya mawasiliano ya Israel iliyoko Rabat ifungwe.

Washiriki wa maandamano hayo walipiga nara kama vile "salamu kwa wanamapambano Gaza," "wananchi wanapinga uhusiano na Israel," "Tunaelekea Al Quds (Jerusalem) tukiwa na mamilioni ya mashahidi," na "watu wanataka ukombozi wa Palestina."

Huko Casablanca, makumi ya maelfu ya Wamorocco pia wameandamana kuelezea mshikamano wao na Gaza na kupinga uhusiano wa kawaida na Israel.

Waandamanaji walisikika wakipiga nara kama vile "Wananchi wa Morocco wanaunga mkono Msikiti wa Al-Aqsa ... na Operesheni ya Kimbunga cha Al-Aqsa," "Wananchi wa Morocco wanapinga uhusiano na Israel," n.k

Mnamo Desemba 2020, Morocco ilianzisha tena uhusiano wa kidiplomasia na utawala haramu Israel hatua ambayo inaendelea kupingwa na wananchi waliowengi katika ufalme huo.

Waandamanaji pia wamepongeza Harakati ya Kiislamu ya Kupigania Ukombozi wa Palestina, Hamas, kwa kuilazimisha Israel ifuate masharti yake katika makubaliano ya kusitisha vita kwa muda ili kufikisha misaada ya kibinadamu Gaza.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live