Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Madereva wa malori wasitisha mgomo wa kusarifirisha mizigo Sudan Kusini

Malori Madereva wa malori wasitisha mgomo kusafirisha mizigo Sudan Kusini

Tue, 7 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Madereva wa malori kutoka Afrika ya Mashariki, wamekubali kusitisha mgomo wao wa wiki mbili wa kutosafirisha mizigo kuelekea kusini mwa Sudan baada ya mamlaka ya nchini humo kuridhia ombi lao la kupata ulinzi wa kijeshi wakiwa njiani.

Maderava hao waligoma kufuatia matukio ya mauaji na utekaji yanayoendelea kutokea katika barabara kuu ya kuelekea nchini humo.

Nae mwenyekiti wa Umoja wa madereva hao, Byron Kinene, amesema kuwa Serikali ya nchini humo imekubaliana na matakwa yao ikiwemo kuwapatia ulinzi kutoka kwa jeshi la polisi.

Kwa upande wa Serikali ya Sudan kusini wao wamethibitisha kuwatimizia madereva na kampuni zote za usafirishaji matakwa walioyawasilisha hasa kuhusu ulinzi na kusema kuwa watahakikisha wanaimarisha ulinzi kwa wadau hao.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live