Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Madereva wa malori wadai kuombwa hongo Kenya

NAMANGA 1 Madereva wa malori wadai kuombwa hongo Kenya

Wed, 10 Jun 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baadhi ya madereva wa malori wanaofanya shughuli zao kupitia mpaka wa Namanga upande wa Keny, wamelalamikia kitendo cha wao kutozwa kiasi cha Shilingi 2000 ya Kenya, ili wakipimwa majibu yao yasikutwe na maambukizi ya Corona.

Malalamiko hayo wameyatoa mbele ya Naibu Waziri wa Afya Dkt Godwin Mollel, wakati akizungumza nao kwa lengo la kusikiliza changamoto zinazowakabili katika kipindi hiki cha janga la Corona.

"Sisi kero yetu, tumekuwa tukipima Kenya tunaambiwa tuna Corona, na mimi wiki mbili nilipima nikapewa cheti nina Corona lakini ukweli ni kwamba sina Corona na sijawahi kutumia dawa yoyote mpaka sasahivi, na tukipimwa tunaombwa 2000 ya Kenya ili watupe majibu kwamba hatuna Corona" amesema Japhet Jeremiah.

Kwa upande wake Dkt Mollel amesema kuwa, Serikali imeliona tatizo lililopo katika mpaka huo na kuweka wazi kuwa, itaongeza kasi katika kuhakikisha inapata suluhu ya changamoto wanazokumbana nazo madereva hao.

"Nimekuja kuwaambia poleni, lakini Serikali yetu itaenda kwa kasi ya ajabu kuhakikisha kwamba hili tatizo lenu katika mpaka huu linatatuliwa" amesema Dkt Mollel.

Mbali na hayo Dkt Mollel amesema kuwa changamoto hii iliyojitokeza katika mpaka wa Namanga ni suala mtambuka, ambalo linahusisha Wizara zaidi ya moja, huku akiweka wazi kuwa suala hili lina uhusiano wa kibiashara na uchumi baina ya nchi hizo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live