Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Madereva malori Malawi waonywa usafirihaji haramu wa binadamu

Madereva Malawiii Malawiii Madereva malori Malawi waonywa usafirihaji haramu wa binadamu

Mon, 28 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Madereva wa malori kusini mwa Afrika ambao wamekuwa wakitumika kusafirisha kiharamu watu au kinyume cha sheria, sasa wanajifunza kuhusu hatari zinazohusiana na shughuli hiyo isiyo halali.

Mafunzo hayo yanatolewa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Madawa ya Kulevya na Uhalifu, UNODC.

Malawi iko katika njiapanda ya misururu kadhaa ya watu wanaokimbia migogoro, ukosefu wa utulivu na umaskini katika Afrika ya Kati na Pembe ya Afrika.

Harakati kama hizo hutoa fursa nzuri kwa wasafirishaji haramu na kwa madereva 5,000 wa malori wa Malawi waliosajiliwa.

Madereva wa malori wanaoishi Malawi sasa wanajifunza kuhusu hatari za kusafirisha wahamiaji na waathiriwa wa usafirishaji haramu wa binadamu, kutokana na mpango unaoungwa mkono na Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kukabiliana na Madawa na Uhalifu (UNODC). Kozi hizo zilizoanza Februari, tayari zinaonekana kuwa na mafanikio.

Wahalifu wanaofanya magendo au kusafirisha binadamu kiharamu ndani ya nchi au kuvuka mipaka hutumia njia zote za usafiri kuwahamisha watu kwa faida na unyonyaji.

Maxwell Matewere, Afisa Mradi wa Kitaifa wa UNODC juu ya usafirishaji haramu wa watu anasema iwapo watakamatwa na mamlaka, madereva wa malori kwa kawaida hukamatwa na kufungwa.

Tangu kuanza kwa kozi za UNODC, Chama cha Madereva Wataalamu kimeripoti kupungua kwa idadi ya kukamatwa kwa madereva wa Malawi kwa tuhuma za ulanguzi wa wahamiaji na usafirishaji haramu wa binadamu.

Mwaka jana, Wizara ya Usalama wa Ndani ya Malawi iliteua kundi jipya la maafisa wa kutekeleza sheria kukabiliana na ongezeko la visa vya ulanguzi wa wahamiaji na biashara haramu ya binadamu.

Tangu Mei, majaribio saba ya biashara haramu ya binadamu na magendo ya wahamiaji yamesimamishwa na mamlaka katika vivuko vya mpaka kutokana na taarifa kutoka kwa madereva wa malori. Kesi ya hivi karibuni ilihusisha Wamalawi 40, wakiwemo watoto, waliokuwa wakichukuliwa kwa malori matatu kuelekea Afrika Kusini na kuzuiwa kwenye mpaka na Zambia.

Hivi karibuni Mamlaka husika za Tanzania zimetangaza kuwa zimekamata lori la mafuta likiwa limewaficha ndani yake wahamiaji haramu 65 wa Ethiopia katika eneo la nyanda za juu kusini.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live