Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Madereva bodaboda waliokuwa wakitafuta petroli ya magendo wauziwa mkorogo

Mafutapiic Nsm Madereva bodaboda

Sun, 20 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Madereva bodaboda wawili wanaosubiri wateja mkabala na Chuo Kikuu cha Kenyatta (KU), wametapeliwa Sh2000 baada ya kuuziwa mkorogo waliodhani ni petroli safi.

Baadaye waligundua kwamba haikuwa ni petroli bali ulikuwa mkorogo wenye sharubati na petroli kiasi ya kufanya uaminike ni mafuta ya ukweli na safi.

Waathiriwa hao walikutana na watu watatu waliokuwa wamebeba vibuyu viwili vya lita kumi-kumi wote wakiabiri pikipiki moja eneo la Bypass Ruiru katika barabara kuu ya Thika.

“Hivyo vibuyu vilikuwa vinaonekana kana kwamba vimejazwa pomoni ikawa rahisi kuwaamini,” mhudumu mmoja akasema.

Kumbe ulikuwa ni mkorogo tu wenye rangi ya petroli ulioongezwa petroli kidogo.

Bodaboda hao wawili wamesema kuwa bei ya juu ya mafuta inewasukuma kushawishika kutafuta soko la magendo la mafuta hayo lakini kikawaramba.

Waliuziwa mkorogo huo Sh100 kwa lita.

Bei ya sasa ya petroli ni Sh195 kwa vituo vingi vya mafuta katika eneo hilo.

Baada ya kununua mafuta hayo, wahudumu hao wa bodaboda wanasema kuwa walifumukana upesi kwa sababu waliamini ni biashara ya magendo kwa hivyo ilihitaji shughuli hiyo kufanywa halahala.

Mmoja wa ‘waliogongwa’ ambaye tunamtambulisha tu kama *AZ, amesimulia jinsi alivyomimina ‘mafuta’ hayo kwenye tanki na kugundua yalikuwa na maji mengi sana na angalau nusu lita ya petroli.

“Wakati wa kununua niliingiza kidole kwenye kibuyu kuthibitisha ni petroli lakini haikusaidia kitu kwani nilitapeliwa,” alisema kwa masikitiko.

Waathiriwa wameambia Taifa Leo kuwa matapeli hao walivaa masurupwenye yaliyoonyesha walikuwa wanafanya kazi ama katika gereji ama kituo cha kuuzia mafuta ili kuwaghilibu.

Japo imebainika hawajaripoti tukio hili kwenye kituo cha polisi, makumi ya wanabodaboda wanaohudumu kwenye maeneo ya hapo Thika Superhighway katika kaunti za Nairobi na Kiambu, wamewatahadharisha wenzao wawe macho.

Aidha, mhudumu mwingine wa bodaboda anaeleza kuwa wamehifadhi mitungi hiyo ya ‘mafuta’ kuwa ithibati ya tukio ili wakati mbiu itapigwa kuwa washukiwa hao wameonekana, wataitoa kama ushahidi kwa maafisa.

Mwanahabari ashambuliwa na wasaidizi wa mbunge wa MaraguaGachagua kwa Odinga: Wewe ni raia binafsi asiyeweza hata...

Chanzo: www.tanzaniaweb.live