Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Madeni EAC yachelewesha taasisi ya fedha

Bb0a556abc5a93d4b5a05fdd3e3a0f8a Madeni EAC yachelewesha taasisi ya fedha

Tue, 21 Jul 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

UCHELEWESHAJI ulipaji wa michango kwa baadhi ya nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) umekwamisha Taasisi ya Fedha na ile ya Takwimu iliyoridhiwa na viongozi wa nchi sita za jumuiya hiyo ili kufi kia mtangamano wake.

EAC ilipitisha itifaki ya Umoja wa Fedha mwaka 2013 na kuridhiwa na wanachama na mchakato kuunda umoja wa fedha unaoendelea kwa kuweka mpango kazi wa miaka 10.

Akizungumza kuhusu changamoto ya utoaji michango ya uanachama iliyosababisha wabunge wa bunge la Afrika Mashariki (EALA) kutaka nchi zisizotoa michango kusitishiwa uanachama, Mwenyekiti wa wabunge wa EALA Tanzania, Dr Abdullah Makame alisema kutotoa michango kunasababisha kazi zao kukwama.

Makame ambaye pia alizungumza kwa niaba ya wabunge wa EALA Tanzania, alisema katika miaka 10 ya utekelezaji inatakiwa kuundwa taasisi mbalimbali ambazo zitasaidia zikiwemo taasisi ya fedha ya Afrika Mashariki na ile ya takwimu zilizopitishwa uundaji wake na bunge Aprili, 2018 April lilipokaa jijini Dodoma.

Pia sheria za kuundwa taasisi hizo zilipata ridhaa kwa wakuu wa nchi lakini kutokana na michango ya bajeti kutotimia na kutoongezeka kwa bajeti malengo ya jumuiya hayafikiwi kutokana na ufinyu wa rasilimali fedha na kutopata rasilimali watu na hivyo kuwa ngumu kufikia malengo ya matangamano wa EAC.

Alisema EAC ina hatua za mtangamano, za Umoja wa forodha, Soko la pamoja na Umoja wa fedha ambapo sasa inashindikana kutekeleza mambo ya msingi na hatua za mtangamano zinakwama kwani wanaotazamiwa kuunganisha jumuiya kuwa soko la pamoja kupata fursa.

Alisema katika utoaji michango hiyo kila nchi inatakiwa kulipa fedha sawa na bajeti hiyo kutumika miezi 12 katika nchi sita hivyo kwa wastani kila nchi inachangia miezi miwili hivyo ikiwa nchi nne pekee zikichangia ni dhahiri kuwa jumuiya itaendeshwa kwa miezi nane tu.

Alisema katika ibara ya 143 na 144 ya jumuiya inataka kila nchi kutoa michango yake na hatua za kuchukua watakachelewesha hivyo bunge walivumilia kwa muda lakini kuna nchi zimeona ni mazoea na kawaida kutolipa michango yao.

Alisema wanawakumbusha baraza la mawaziri kutumia busara zao kuwakumbusha viongozi wa nchi kuwashurutisha wasiolipa walipe madeni Alitoa mfano Sudan Kusini ni mwanachama AU na ilikuwa haijalipa michango yake kwa miaka mitatu na kusitishiwa mshahara lakini hata wiki moja haikupita wakalipa na hata mwaka jana asasi ya kiraia zilipopeleka malalamiko bunge la EALA na kufika kwa Spika na bunge kujadili hazikufika siku 10 walilipa dola milioni 300.

Chanzo: habarileo.co.tz