Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Madaktari wasio na mipaka wafukuzwa Sudan

Madaktari Wasio Na Mipaka Madaktari wasio na mipaka wafukuzwa Sudan

Mon, 1 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shughuli za Madaktari Wasio na Mipaka zimesitishwa katika Jimbo la Al Jazirah nchini Sudan kutokana na kuendelea kuwa mbaya hali ya usalama katika jimbo hilo.

Takriban wiki mbili zilizopita, vikosi vya radiamali ya haraka RSF viliuteka mji wa Wad Madani, mji mkuu wa jimbo la Al-Jazirah, kusini mwa jimbo la Khartoum, Sudan.

Vyombo vya habari vya Sudan pia vimeripoti kuuawa raia na kuporwa mali zao na vikosi vya RSF.

Kuhusiana na jambo hilo, Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa watu zaidi ya 300,000 wa jimbo la Al Jazirah wamekuwa wakimbizi, na kamati ya madaktari ya Sudan pamoja na kuomba msaada kwa mashirika ya kimataifa, imetaja hali ya afya katika jimbo hilo ni mbaya sana.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Tasnim, shirika la Madaktari Wasio na Mipaka limetangaza katika taarifa kuwa watu wenye silaha walishambulia jengo lake katika mji wa Wad Madani na kuiba magari mawili pamoja na vitu vingine vilivyokuwemo katika jengo hilo. Wakazi wa Wad Madani wakihama mji wao

Likiashiria kutekwa jimbo la Al-Jazirah na vikosi vya RSF, shirika hilo lilibainisha wiki iliyopita, kwamba hali ya usalama katika jimbo hilo ilizidi kuwa mbaya na kulazimika kusimamisha shughuli zake katika mji wa Wad Madani na kuwahamishia wafanyakazi wake katika maeneo salama nchini Sudan na nchi jirani.

Huku wakielezea kusikitishwa na kutopata wakazi wa Wad Madani huduma chanya za matibabu na dawa, Madaktari Wasio na Mipaka walivitaka vikosi vya RSF kuanda uwanja salama kwa raia kunufaika kirahisi na huduma za afya na matibabu.

Shirika la Afya Duniani pamoja na kuelezea kuenea magonjwa ya kuambukiza na uhaba wa chakula nchini Sudan, limetaka kuongezwa misaada ya kifedha ili liweze kutoa huduma za afya na tiba zinazohitajiwa na wananchi wa Sudan.

Tangu Aprili 15, 2023, Sudan imekuwa ikishuhudia vita vya kuwania madaraka kati ya jeshi la nchi hiyo na vikosi vya RSF.

Ofisi ya Umoja wa Mataifa inayoshughulikia Masuala ya Kibinadamu (OCHA) ilitangaza siku chache zilizopita kuwa zaidi ya watu elfu 12 wameuawa nchini Sudan kutokana na vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live