Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Madaktari waanza mgomo Kenya

Mtanzanianews 131975371 426781715364276 9015138192819703176 N Madaktari waanza mgomo Kenya

Tue, 22 Dec 2020 Chanzo: millardayo.com

Madaktari wanaofanya kazi katika hospitali za serikali nchini Kenya, wameanza mgomo wa kote nchini, wakilalamikia kutopewa bima ya afya, na ukosefu wa vifaa vya kujikinga na maambukizi ya virusi vya corona wanapowashughulikia wagonjwa walioambukizwa virusi hivyo.

Mgomo huo umeanza jana baada ya muungano wa madaktari, wanafamasia na madaktari wa meno kusema kwamba serikali imekosa kushughulika mahitaji yao kwa mda wa miezi nane iliyopita.

Muungano huo umesema kwamba serikali ya Kenya imepuuza maslahi ya wafanyakazi wa afya nchini humo.

Kulingana na muungano huo, madaktari 14 wamekufa kutokana na virusi vya Corona nchini Kenya, tangu kisa cha kwanza kiliporipotiwa mwezi Machi mwaka huu.

Mgomo huo ulikuwa umepangiwa kuanza Desemba 7, lakini ukaahirishwa kwa muda wa wiki mbili ili kuruhusu mazungumzo kati ya viongozi wa madaktari na serikali, kufanyika.

NABII ANAEDAIWA KUMPANGA MUUMIN APIGE KELELE, MLEVI ALIEJIFUNGULIA BAR

Chanzo: millardayo.com