Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Madaktari Nigeria warejea baada ya mgomo wa miezi miwili

Doctorrrrrrr Warejea baada ya mgomo wa miezi miwili

Wed, 6 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Madaktari wa hospitali za serikali nchini Nigeria wamerejea kazini baada ya miezi miwili ya mgomo mkubwa kuwahi kutokea nchini humo, Madaktari hao wamekuwa wakipigania ongezeko la mishahara, mafao na vifaa vya kazi.

Chama cha Madaktari nchini humo, NARD, ambacho kinawakilisha asilimia 40 ya madaktari wote, kimesema kuwa tayari suala la malipo limetatuliwa hivyo kesho madaktari wote watarejea kazini.

Taifa hilo lenye watu wapatao milioni 210, ina jumla ya madaktari 42,000 huku madaktari 16,000 kati yao ni wanafunzi, hii inapelekea tafa hilo kuw ana uhaba wa wataalamu wa afya katika baadhi ya hospitali hasa za vijijini.

Mgomo huo ulifanyika wakati taifa hilo lenye watu wengi zaidi barani Afrika likiwa linapambana na janga la UVIKO-19, na inaelezwa kuwa hadi sasa, watu 200,000 wameambukizwa virusi vya corona, ambapo 2,720 wamepoteza maisha.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live