Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Madaktari Kenya waendelea na mgomo

Madaktari Kenya Kenyaaa Madaktari Kenya waendelea na mgomo

Wed, 10 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Madaktari katika Kaunti ya Mombasa nchini Kenya wamepuuzilia mbali ombi la serikali la kurudi kazini ili kukabiliana na mlipuko wa ugonjwa wa nimonia miongoni mwa watoto.

Jumatatu iliyopita, serikali ya Kaunti ya Mombasa iliwaamrisha madaktari na maafisa wa kliniki walio likizoni na wale wanaoendeleza mgomo wao wa kitaifa kurudi kazini mara moja, ili kukabiliana na mlipuko wa nimonia baina ya watoto.

Hata hivyo, wakuu wa chama cha madaktari nchini Kenya tawi la Pwani wamekataa wito huo, wakisema mgomo huo uliitishwa na afisi yao ya kitaifa.

Madaktari wa watoto katika Kaunti ya Mombasa wanasema, hospitali za watu binafsi zimekuwa zikitibu watoto wanaougua nimonia huku wengi wao wakilazwa katika vyumba vya wagonjwa mahututi kufuatia kudhohofika kwa hali yao ya afya.

Taarifa zinasema, ongezeko la idadi ya wagonjwa hao linazidi kuwatia wasiwasi maafisa wa afya katika kaunti hiyo.

Hali hii inazidi kuwa mbaya kutokana na mgomo wa kitaifa wa madaktari nchini Kenya.

Daktari wa watoto wa Hospitali ya Aga Khan mjini Mombasa, Dkt Hemed Twahir, alisema katika kipindi cha mwezi mmoja uliopita, wamekuwa wakiuguza maradhi ya nimonia na kuendesha miongoni mwa watoto. "Tumelazimika kuwalaza katika chumba cha wagonjwa mahututi kwa sababu ya kudhoofika kwa afya,” alisema Dkt Twahir.

Daktari huyo aliwasihi wazazi kuhakikisha watoto wanaoshwa mikono kwa sabuni mara kwa mara, wanakunywa maji safi yaliyochemshwa au kutiwa dawa.

Madaktari nchini Kenya wamesitisha kutoa huduma za dharura katika hospitali za serikali na hivyo kuutumbukiza mfumo wa afya katika mgogoro mkubwa zaidi.

Muungano wa Madaktari, Wafamasia na Madaktari wa Meno nchini Kenya (KMPDU) umechukua uamuzi wa kusitisha huduma za dharura huku madaktari wakiitaka serikali kushughulikia malalamiko yao hasa kuhusu ucheleweshaji wa kuajiri wahudumu wa afya.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live