Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mackenzie aomba auliwe na mwili wake utupwe mtoni

Mackenzie Aliwasifu Wafuasi Wanaokufa Kama Mashujaa Mackenzie aomba auliwe na mwili wake utupwe mtoni

Thu, 10 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchungaji Paul Mackenzie wa kanisa la Good News International la nchini Kenya, ambaye anahusishwa na vifo vya zaidi ya watu 400, ambao ni waumini wa kanisa lake, baada ya kuwashawishi kufunga hadi kufa, huko Shakahola katika Kaunti ya Kilifi, ameimbia mahakama nchini humo kuwa kama haitaki kumpa haki yake ya dhamana, imuue na mwili wake utupwe mto Yala.

Mchungaji huyo ameyasema hayo katika mahakama ya Shanzu, huku akilia na kulalamika kuwa haki zake na za washtakiwa wenzake wengine 15 zimekuwa zikikiukwa wakati wakiwa kizuizini, na kudai kuwa amekaa siku mbili bila kula na kuoga na kwamba amekuwa akifungiwa kwenye chumba chenye giza.

Hata hivyo, Mwendesha mashtaka ameomba Mchungaji huyo aendelee kuzuiliwa kwa siku 47 zaidi ili kukamilisha uchunguzi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live