Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mackenzie akabiliwa na mashtaka ya ugaidi kufuatia mauaji ya Shakahola

Mchungaji Mackenzie Na Wenzake Kuendelea Kushikiliwa Kwa Mwezi 1 Zaidi Mackenzie akabiliwa na mashtaka ya ugaidi kufuatia mauaji ya Shakahola

Wed, 17 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Afisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma nchini Kenya, (ODPP) imetangaza kwamba imefanikiwa kupata ushahidi wa kutosha wa kuwashtaki washukiwa 95 wa mauaji ya Shakahola katika kaunti ya Kilifi eneo la pwani.

Taarifa ya ODPP imesema, imepokea faili ya uchunguzi wa kina ulioongozwa na kitengo cha upelelezi wa makosa ya jinai (DCI).

Baada ya maafisa wa ODPP kuzipitia faili hizo, wamepata kwamba ushahidi uliokusanywa unatosha kuwafungulia mashtaka washukiwa hao. Makosa ya watu hao yameorodheshwa chini ya sheria ya kuzuia ugaidi ya mwaka 2012 pamoja, ile ya kuzuia uhalifu wa kupangwa ya mwaka 2010, sheria ya watoto ya mwaka 2001, sheria ya kuzuia unyanyasaji ya mwaka 2017 na sheria ya elimu ya msingi ya mwaka 2013.

Wafuasi hao wa dhehebu la Kikirito lenye misimamo mikali wanatuhumiwa kwa mauaji, kuua bila kukusudia, kunyanyasa, kuwasababishia watu madhara mwilini, kujihusisha na uhalifu uliopangwa, kueneza itikadi kali, kufanikisha vitendo vya kigaidi na kadhalika. Kasisi mwenye misimamo mikali Paul Mackenzie akiwa mahakamani

Afisi hiyo ya mkurugenzi wa mashtaka ya umma sasa imeagiza kwamba washukiwa wafikishwe kwenye Mahakama Kuu au mahakama nyingine ikiahidi kuendesha kesi hizo haraka. Wakenya wamekuwa wakisubiri kwa hamu hatima ya kesi hiyo ya mauaji ambayo yaliitikisha nchi.

Shakahola ni eneo la msitu linalopatikana huko Malindi katika Kaunti ya Kilifi, ambapo mhubiri tata wa Kikristo mwenye misimamo mikali, Kasisi Paul Nthenge Mackenzie alikuwa akiendesha shughuli zake pamoja na wafuasi wake.

Anasemekana kuhimiza wafuasi wake kufunga kula na kunywa ili waage dunia ili eti waende kumuona Nabii Isa (Yesu). Idadi kubwa ya wafuasi wa kanisa hilo walipoteza maisha kwa kufuata agizo hilo.

Mackenzie na wafuasi wake kadhaa walikamatwa mwaka jana mwezi Aprili na wamekuwa kizuizini tangu wakati huo ili kutoa nafasi kwa uchunguzi.

Miili ya watu 429 wakiwemo watoto imefukuliwa kutoka maeneo ya makaburi huko Shakahola na uchunguzi umebaini kuwa mbali na kufa njaa wengine wakibainika kupoteza maisha kupitia kunyongwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live