Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Machafuko yasababisha maelfu kuyakimbia makaazi yao nchini Msumbiji

Msumbijiiiii Nchii Machafuko yasababisha maelfu kuyakimbia makaazi yao nchini Msumbiji

Fri, 23 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Maelfu ya raia wamelazimika kuyakimbia makazi yao nchini Msumbiji baada ya kuibuka tena machafuko kaskazini mwa nchi hiyo.

Takwimu zilizotolewa na Umoja wa Mataifa zinaonyesha kuwa, wimbi jipya la machafuko yanayotokana na uasi kaskazini mwa Msumbiji, yamesababisha maelfu ya watu kukimbia makaazi yao katika mkoa wa Cabo Delgado.

Tahadhari iliyotolewa na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia uhamiaji IOM imesema mashambulizi ya hivi karibuni katika mikoa ya Macomia, Chiure na Mecufi yamesababisha watu 13,088 kupoteza makaazi yao. Wengi wa waliokuwa wanatoroka maeneo hayo ya machafuko ni watoto waliotumia mabasi, maboti na hata wengine kutembea kwa miguu, kukimbilia mahali salama.

Rais wa Msumbiji Filipe Nyusi amethibitisha kwamba, kumekuwepo na wimbi jipya la watu wanaoitoroka nchi, lakini alisisitiza kwamba maafisa wa usalama wameidhibiti hali hiyo. Magaidi wa Daesh nchini Msumbiji

Kulingana na msemaji wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuwashughulikia wakimbizi UNHCR mwezi uliopita kulikuwa na idadi ya makundi ya wanamgambo waliojihami Kusini mwa mji wa Cabo Delgado.

Mashambulizi ya makundi ya kigaidi na kundi la kigaidi la ISIS au Daesh huko Cabo Delgado yameua maelfu ya watu tangu mzozo ulipozuka mwaka wa 2017, na kuvuruga miradi ya mabilioni ya dola ya gesi asilia na uchimbaji madini.

Machi mwaka 2021 magaidi nchini Msumbiji waliuteka mji wa Palma wa kaskazini mwa nchi hiyo ulioko katika mpaka wa nchi hiyo na Tanzania, na kuua makumi ya watu na kuwalazimisha kuwa wakimbizi watu wengine zaidi ya 50,000. Eneo hilo limekumbwa na uasi baada ya kuanza mradi wa gesi wa dola bilioni 20.

Mwezi Julai mwaka 2021 Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika SADC ilianza kutuma wanajeshi wake kulisaidia jeshi la Msumbiji kupambana na magaidi waliojizatiti kaskazini mwa nchi hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live