Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mabondia wa Tanzania wachezea kichapo Latvia

95152 Mabondia+pic Mabondia wa Tanzania wachezea kichapo Latvia

Mon, 10 Feb 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

MBONGO buana huwa haishiwi visingizio, kwani unaambiwa mabondia wawili wa Tanzania, Jonas Segu na Imani Daud, waliopigwa nchini Latvia hajakosa cha kujitetea juu ya vipigo hivyo vya pointi. Mabondia hao walipigwa usiku wa kuamkia leo katika mapambano yalichezwa kwenye ukumbi wa Arena Riga huko Riga. Segu alichapwa na Vahram Vardanyan kwa pointi za majaji 2-1 katika uzani wa Light, huku Daud akinyooshwa na Nikita Smirnovs kwa majaji wote watatu. Kocha aliyeambatana nao nchini humo, Emmanuel Mlundwa alisema Daudi alipigwa kwa tofauti ya pointi nyingi wakati Segu alicheza kwa kiwango bora licha ya majaji kumbeba mpinzani wake. "Kwa Segu kucheza ugenini ndiko kumemponza na majaji kuamua kumpa ushindi mzungu, ila Daudi amepigwa kwa kukosa uzoefu wa mapambano ya kimataifa, amepigwa na bondia ambaye anachipukia lakini alimzidi kasi na mbinu," alisema Mlundwa nyota wa zamani wa kimataifa wa ngumi. Alisema ushindi wa pointi kwa yeyote anaweza kupew na imetokea kwa Watanzania hao ambao wote walicheza na kumaliza raundi na majaji kuamua matokeo yao. Mabondia hao watarejea nchini keshokutwa.

Chanzo: mwananchi.co.tz