Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mabomu yaipiga Somalia kabla ya mkutano wa viongozi wa Afrika Mashariki

Mabomu Yaipiga Somalia Kabla Ya Mkutano Wa Viongozi Wa Afrika Mashariki Mabomu yaipiga Somalia kabla ya mkutano wa viongozi wa Afrika Mashariki

Wed, 1 Feb 2023 Chanzo: Bbc

Milipuko ya mabomu imelipuka katika mji mkuu wa Somalia Mogadishu, huku viongozi wa kikanda wakikusanyika katika mji ho kujadili mashambulio ya pamoja dhidi ya Kundi la wanamgambo wa Al shaabab.

Milipuko minne ilipiga maeneo yaliyopo karibu na kasri la rais lenye ulinzi mkali.

Hakuna taarifa kuhusu majeruhi.

Viongozi wa Kenya, Ethiopia na Djibouti wanafanya mkutano huko Jumatano kufuatia jeshi la Somalia kuyateka hivi karibuni maeneo yaliyokuwa yamenyakuliwa na wanamgambo wa Alshaabab.

Al-Shabab bado wanadhibiti eneo kubwa la Somalia, na bado wanafanya mashambulio katika maeneo mbali mbali ya Somalia, ukiwemo mji mkuu Mogadishu

Lakini wamepoteza eneo tangu serikali , inayosaidiwa na vikosi vya Marekani na vya Kiafrika kufanya mashambulio mwezi Agosti.

Chanzo: Bbc