Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mabomu ya machozi yatumika kutawanya waandamanaji Sudan

Machozi Sudan Mabomu ya machozi yatumika kutawanya waandamanaji Sudan

Wed, 5 Jan 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Makundi yanayounga mkono demokrasia nchini Sudan yameitisha maandamano makubwa ya kupinga mapinduzi hii leo, mnamo wakati taifa hilo likizidi kutumbukia katika machafuko ya kisiasa, baada ya kujiuzulu kwa waziri mkuu.

Waandamanaji walikuwa wakipiga kelele za kukataa utawala wa kijeshi, na kutoa madai ya kuvunjwa kwa baraza tawala la Sudan linaloogozwa na Jenerali Abdel Fattah al-Burhan, alieongoza mapinduzi ya Oktoba 25 na kuuondoa utawala wa mpito wa kiraia.

Maelfu ya waandamanji wameshuhudiwa kote Sudan, ikiwemo katika mji mkuu Khartoum na mji wake pacha wa Omdurman pamoja na mji wa mashariki wa Port Sudan, kadhalika katika mji wa Darfur Kusini wa Nyala.

Waziri Mkuu Abdalla Hamdok alipinduliwa katika mapinduzi ya Oktoba, lakini alirejeshwa madarakani baada ya mwezi mmoja kufuatia makubaliano na jeshi yaliotafuta kutuliza mzozo na maandamo ya kupinga mapinduzi.

Hamdok aliachia nafasi hiyo siku ya Jumapili kufuatia mkwamo wa kisiasa, akisema alishindwa kupata muafaka kati ya majenerali wanaotawala na vuguvugu la kutetea demokrasia.

Sudan imedhoofika kisiasa tangu mapinduzi ya Oktoba 25, yaliofanyika miaka mwili baada ya uasi wa umma uliolaazimisha kuondolewa madarakani kwa kiongozi wa muda mrefu wa taifa hilo Omar al-Bashir na serikali yake inayoegemea mrengo wa kidini mwezi Aprili 2019.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live