Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mabilioni yaliyoibiwa na Makamu wa Rais Guinea kutumika kununua chanjo

Makamu Guinea Teodorin Nguema Obiang Mangue, Makamu wa Rais Guinea

Tue, 21 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Idara ya Haki ya Marekani imesema kuwa kiasi cha dola milioni 26.6 sawa na shilingi bilioni 60.29 za Tanzania zilizokamatwa kutoka kwa Makamu wa rais wa Guinea, Teodorin Nguema Obiang Mangue, zitatumika kutoa na kusambaza Chanjo ya Uviko-19 pamoja na kuratibu shughuli nyingine za kiafya katika ukanda wa Afrika Magharibi.

Hatua hii imefikiwa ikiwa ni pamoja na Makamu huyo kutakiwa na mamalaka hiyo kuuza jumba lake la kifahari lilipo katika mji wa California, gari aina ya Ferrari na vito vingine vya thamani, mali ambazo anatajwa kuzimiliki tangu aingie Marekani mwaka 2014 akiwa ana tuhumiwa kuhusika katika sakata la rushwa pamoja na utakatishaji fedha madai ambayo alikana kuhusika nayo.

Hata hivyo Maafikiano hayo yanabainisha kiasi cha dola 10.3 sawa na shilingi bilioni 23.19 za Tanzania zitakazo patikana katika mauzo ya mali hizo zitapekelekwa katika mamlaka za nchini Marekani huku kiasi kinachosaliwa kutolewa kama msaada kwa kufanikisha zoezi la ugawaji wa chanjo pamoja na kuboresha sekta ya afya.

Umoja wa Mataifa unatarajiwa kupokea kiasi cha dola 19 sawa na shilingi bilioni 44.06 za kitanzania ambazo zitatumika kununua chanjo itakayotumika kuchoma watu takribani laki sita walio katika ukanda huo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live