Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mabilioni yaahidiwa kwa bara la Afrika kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa

Bankmoon.png Mabilioni yaahidiwa kwa bara la Afrika kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa

Wed, 6 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakuu wa nchi mbalimbali barani Afrika na viongozi wa taasisi mbalimbali za Kimataifa, wamekuwa wakihutubia katika kongamano la Mazingira kuhusu bara la Afrika, ambalo linatamatika hivi leo jijini Nairobi nchini Kenya.

Serikali ya Falme za Kiarabu itakayokuwa mwenyeji wa mkutano wa Umoja wa Mataifa wa COP 28 mwezi Novemba, imeahidi kutoa Dola Bilioni 4.5 ili kufadhili miradi ya kuzalisha nishati safi barani Afrika, kusaidia kupambana na mabadiliko ya tabia nchi.

Tutatoa dola bilioni 4.5 za Marekani ambazo zitachangia katika dola bilioni 12.5 za ziada kutoka kwenye vyanzo vya kimataifa vya umma na kibinafsi. Ni matarajio yentu kwamba hatua hii itaanzisha upya ushirikiano wa mageuzi na kuzindua matumaini ya kuinua mradi wa nishati safi kati bara hili muhimu. Amsema Sultan Al Jaber, Mkuu wa kampuni ya taifa ya mafuta ya Falme za Kiarabu.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres naye amepata fursa ya kuhotubia mkutano huo, na kuyataka mataifa tajiri duniani, kutimiza ahadi yao ya kupunguza uzalishaji wa hewa chafu na kulisaidia bara la Afrika, kukumbatia nishati jadidifu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live