Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mabilioni ya Kenyatta yabainika kufichwa Uingereza

RTX7Z7J4 730x419 Mabilioni ya Kenyatta yabainika kufichwa Uingereza

Mon, 4 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Uchunguzi uliofanywa na Jumuiya ya Kimataifa ya Wanahabari wa Upelelezi ICIJ, umebaini kuwa Wakuu wa nchi na Serikali kutoka mataifa ya Azerbaijan, Kenya na Jamuhuri ya Czech wanadaiwa kuficha mali zenye thamani ya mamilioni ya dola nchini Uingereza.

Uchunguzi huo maarufu kama "Pandora Papers" unaojumuisha waandishi wa habari 600 kutoka katika vituo vya Washington Post, BBC na The Guardian, ulijikita zaidi katika hati milioni 11.9 zilizovuja kutoka katika taasisi 14 za kifedha duniani.

Jumla ya viongozi 35 wa sasa pamoja na wale wa zamani wameorodhesha katika orodha hii iliyochambuliwa vilivyo na ICIJ huku wakishutumiwa kuhusika na vitendo vya rushwa, uhujumu uchumi pamoja na kukwepa kodi.

Kitendo cha Kenya kutajwa katika orodha hii kimeibua maswali mengi huku wengi wakihoji juu ya harakati za Rais Uhuru Kenyatta za kupambana na rushwa ili hali yeye akiwa mmoja wa washukiwa wa vitendo hivyo.

Kwa nchi za Afrika, taarifa hizo zimebainisha Rais Kenyatta na nduguze wana utajiri wa zaidi ya dola milioni 30(takribani Tsh Bilioni 70) jijini London, Uingereza.

Ripoti hii imenukuliwa ikisema kuwa kwa ni aibu kwa viongozi wanaopinga rushwa , wanaohamasisha kuhusu kulipa kodi, pamoja na kuhimiza uwekezaji wa ndani kutajwa katika orodha hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live