Viongozi wa nchi za Afrika wameombwa kutumia nafasi zao kusaidia kuendesha mazungumzo ya amani yatakayowezesha kumaliza mapigano yanayoendelea katika nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na nchi nyingine za Afrika.
- Wito huo umetolewa na Mabalozi wa amani kutoka nchi za Kenya na Tanzania katika maandamano ya hisani kuhamasisha amani yaliyoandaliwa na taasisi ya kidini ya Pan African Christian Foundation for Evangelization Assistance (PACFEA), yenye makao yake makuu nchini Marekani.
- Dk. Kenedy Waningu, Balozi wa amani nchini Kenya kutoka chuo cha Kimataifa cha amani kilichopo Florida nchini Marekani alisema kuwa mazungumzo baina ya pande mbili zinazopingana ndiyo silaha pekee inayoweza kumaliza vita baina ya vikundi vinavyopigana katika nchi za Afrika.