Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mabalozi 13 waitaka serikali na upinzani Kenya kujadiliana

Rais Ruto, Naibu Wake Na Wabunge Kuongezwa Mishahara   SRC Mabalozi 13 waitaka serikali na upinzani Kenya kujadiliana

Tue, 18 Jul 2023 Chanzo: Bbc

Wanadiplomasia wakiwemo mabalozi kutoka mataifa 13 ya kigeni wenye balozi zao nchini Kenya wameonyesha wasiwasi wao kuhusu mauaji na ghasia nchini Kenya wakati wa Maandamano.

Kulingana na taarifa ya pamoja iliotumwa kwa vyombo vya habari , mabalozi hao kutoka Marekani na mataifa ya magharibi wameshtumu matumizi ya risasi Pamoja na uharibifu wa mali wakati wa maandamano ya hivi majuzi.

Badala yao viongozi hao sasa wamewataka viongozi wa upinzani Pamoja na wale waserikali kuwasilisha matakwa yao kupitia majadiliano ya kuleta amani ili kutafuta suluhu ya kudumu kwa lengo la kuhakikisha kuwa hakuna maafa Zaidi.

Wameongezeaema kwamba wako tayari kusaidia juhudi za kupata suluhu ya haraka.

Matamashi yao yanajiri huku upinzani ukitarajiwa kuongoza maandamano ya siku tatu dhidi ya serikali kuanzia kesho Jumatano hadi Ijumaa kuishinikia kufutilia mbali muswada wa fedha 2023.

Siku ya Jumatano iliopita takriban watu sita waliuawa wakati wa maandamano yaliofanyika nchi nzima kupinga hatua ya rais William Ruto kuunga mkono muswada huo unaoshinikiza kuongezwa kwa kodi .

Upinzani umeapa kutositisha maandamano hayo ambayo yamesababisha uharibifu mkubwa wa mali hadi serikali iangazie masuala ya kupanda kwa gharama ya maisha, uundaji wa tume mpya wa IEBC kwa ushirikiano na upinzani mbali na ukaguzi wa seva ya matokeo ya uchaguzi mkuu wa mwaka jana.

Chanzo: Bbc