Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mabaki ya Rais wa zamani wa Burundi Pierre Buyoya yarejeshwa Burundi

Gfdtfcytfytcv Pierre Buyoya

Wed, 17 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mabaki ya Rais wa zamani wa Burundi Meja Pierre Buyoya yamerejeshwa Burundi katika nchi aliyozaliwa miaka minne baada ya kufariki Dunia nchini Ufaransa na kuzikwa Mali.

Mabaki hayo yamewasili na ndege ya Shirika la Ethiopian Airline katika Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Melchior Ndadaye mjini Bujumbura majira ya saa tisa zaa alasiri.

Taarifa kutoka katika familia ya hayati Rais Pierre Buyoya zinasema kuwa hakuna kiongozi kutoka serikalini aliyehudhuria katika mapokezi ya mabaki hayo kwenye uwanja wa Ndege.

Mabaki ya Rais huyo wa zamani wa Burundi yataweza kuzikwa kwa heshima katika kijiji cha Rutovu mkoani Bururi mashariki mwa nchi alipozaliwa.

Rais Buyoya (71), alifariki Dunia Oktoba 17, 2020 nchini Ufaransa kwa ugonjwa wa Corona na kwenda kuzikwa nchini Mali alipokuwa mjumbe maalumu wa Umoja wa Afrika.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live