Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mabadiliko ya jina Nigeria ";lirudiwe kupitishwa"

Screenshot 2021 06 04 At 10.45.04 660x400.png Mabadiliko ya jina Nigeria ";lirudiwe kupitishwa"

Fri, 4 Jun 2021 Chanzo: millardayo.com

Mjadala wa kutaka jina la Nchi ya Nigeria libadilishwe umeendelea kuwa gumzo nchini humo wakati huu ambapo Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wanaendelea kukusanya mapendekezo ya kubadili Katiba, hii ni baada ya Raia mmoja aitwaye Adeleye Jokotoye kupendekeza jina la Nchi hiyo kuwa United African Republic (Jamhuri ya Muungano Afrika).

Jokotoye amesema sababu ya kuomba jina lirudiwe kupitishwa upya ni kwakuwa jina hilo ni la Kikoloni ambalo wakati linapitishwa yeye hakuwepo halikupendekezwa kwa matakwa ya Wanaigeria ila llilipendekezwa karne ya 19 na Mwandishi wa Habari wa Uingereza, Flora Shaw, ambaye baadaye aliolewa na Msimamizi wa Kikoloni, Frederick Lugard.

Bashir Ahmad ambaye ni Msaidizi wa Rais wa Nigeria amesema anashangazwa kuona Watu wameanza kumtupia lawama Rais Muhammadu Buhari wa Nchi hiyo kuhusu mapendekezo hayo wakati aliyependekeza ni Raia na wala sio Rais wala sio Serikali.

RAIS SAMIA ASHTUKIZA SOKONI KISUTU, AKUTA MADUDU, AMBANA MSIMAMIZI “UNA UHAKIKA”

Chanzo: millardayo.com