Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mabadiliko Tabia Nchi yanaathiri zaidi Afrika

Athari Mabadiliko Tabianchi Mabadiliko Tabia Nchi yanaathiri zaidi Afrika

Tue, 29 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waandishi wa habari kutoka nchi za Afrika wametakiwa kuandika habari zinazohusu mabadiliko ya tabia nchi ili kuhamasisha hatua muhimu za mabadiliko katika jamii ikiwemo utunzaji wa mazingira na mabadiliko ya kisera.

Septemba 4 hadi 6 mwaka huu Afrika inatarajia kufanya mkutano mkubwa wa mabadiliko ya tabia ya nchi katika jiji la Nairobi nchini Kenya.

Akizungumza wakati wa mafunzo kwa waandishi wa habari zaidi ya 40 kutoka mataifa 30 ya Afrika ,Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika lisilo la kiserikali la Power Shift Africa, Mohamed Adow amesema mafunzo hayo yanalenga kuwaongezea uwezo waandishi wa habari ili kujua mabadiliko ya tabia nchi na kuelimisha jamii.

Aidha amesema kuwa vyombo vya habari ni muhimu kusaidia jamii kuelewa masuala ya mabadiliko ya hali ya hewa na kuchukua hatua zinazohitajika

“ Kutokana na mabadiliko ya tabia nchi Afrika inaathirika zaidi kuliko mabara mengine kwani tunashudia ukame na watu kukosa chakula,ongezeko la joto ,mabadiliko ya misimu yasiyotarajiwa na mengine lakini uandishi wa mabadiliko ya tabianchi bado ni mdogo,"ameeleza.

Amesema kuwa vyomba vya habari vinawajibu wa kuelimisha jamii ili iweze kuchukua hatua thabiti za kukabiliana na mabadiliko hayo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live