Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Maandamano yaigharimu Kenya hasara Sh3 bilioni

Daktari Kenya: Nilitibu Watoto Waliopigwa Mabomu Ya Kutoa Machozi Bure Maandamano yaigharimu Kenya hasara Sh3 bilioni

Fri, 14 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakati sasa hali ikionekana kurejea katika utulivu baada ya vumbi kumtika kutokana na ghasia zilizozuka wakati wa maandamano yaliyofanyika nchi nzima siku ya Jumatano Julai 12, 2023; wafanyabiashara sasa wanahesabu hasara ya Sh3 bilioni.

Hasara hiyo ni kama Sh49 bilioni za tanzania, ambapo Muungano wa Sekta ya Kibinafsi nchini humo (Kepsa), umesema imetokana na kufungwa kwa biashara wakati wa maandamano, lakini pia imesababishwa na vitendo vya uporaji na uharibifu wa mali.

Julai 12, 2023; kulifanyika maandamano yaliyoitishwa na Kambi ya Upinzani nchini humo kwa lengo la kupinga kupanda kwa gharama za maisha, na miji iliyokubwa na ghasia na hivyo kusababisha hasara hiyo ni pamoja na Nairobi, Nakuru, Kisumu, Mombasa, Machakos na Kisii.

Kwa mujibu wa mtandao wa Nation Kenya, imeelezwa kuwa hasara hiyo inaweza kuwa mbaya zaidi wiki ijayo, iwapo kambi hiyo itaendelea na tishio lake la kuitisha maandamano ya kila Jumatano ya wiki, jambo ambalo wataalam wa uchumi wanasema litalemaza shughuli za kibiashara na kusababisha hasara ya mabilioni ya shilingi.

Hapo awali, Upinzani ulikuwa umetishia kufanya maandamano siku tatu kwa wiki.

"Kuanzia wiki ijayo, tutakuwa na siku tatu za maandamano kuanzia Jumatatu hadi Jumatano hadi Rais Ruto asikilize Wakenya," alisema Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna jana.

Biashara kuanzia huduma za usafiri wa umma, biashara ndogondogo, uzalishaji, biashara za rejareja, na hoteli, ni miongoni shughuli ambazo zimekubwa madhara makubwa ya maandamano na hivyo kupoteza tija.

Hasara hiyo imeigusa hata sekta ya umma, ambapo mali za umma kama vile magari ya polisi, ofisi za Serikali na miundombinu ikihusisha ‘Nairobi Expressway’ iliyojengwa na Wachina kwa ubia kati ya sekta ya umma na ile ya binafsi (PPP), imeharibiwa na hatimaye hasara hiyo itabebwa na walipa kodi.

Jana Waziri wa Uchukuzi, Kipchumba Murkomen, amesema kuwa chini ya makubaliano ya Kenya na Moja Expressway, kampuni tanzu kutoka China inayoiendesha barabara hiyo, walipa kodi wanapaswa kulipia gharama ya uharibifu ndani ya siku 28.

"Uharibifu uliofanywa kwa Expressway katika kipindi hicho kifupi unaweza kuwa dola milioni 5 (Sh707 milioni)," amesema waziri huyo.

Kwa upande mwingine, Chama cha Wafanyabiashara wa Rejareja nchini (Retrak), kimesema kushuka kwa mauzo yao kwa wastani wa asilimia 30, na uporaji wa bidhaa za thamani ambayo bado haijajulikana, sekta hiyo imepoteza hadi Sh1.2 bilioni.imeripotiwa

"Tuliripoti kupungua kwa mauzo hadi asilimia 30. Tunakadiria gharama ya ghasia hizo ilikuwa kati ya Sh920 milioni na Sh1.2 bilioni katika maduka makubwa ya kisasa na ya jumla,” alisema Mtendaji Mkuu wa Retrak, Wambui Mbarire.

Huku watu wakibaki majumbani, Chama cha waendesha Magari ya Usafiri wa Umma (PSVs), wanakadiria kupata hasara ya takriban Sh1 bilioni huku maelfu ya madereva na wapiga debe, hasa wanaolipwa kwa siku, wamerudi nyumbani bila chochote.

“Wanachama wetu walilazimika kuegesha magari yao kwa sababu hakukuwa na abiria. Hili likiendelea, wanachama wetu wengi watashindwa kulipa mikopo, jambo linaloweza kuwafanya wakapoteza magari yao,” amesema Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki wa Matatu (MOA) Albert Karakacha.

Kwa upande mwingine, Mwenyekiti wa Chama cha Mitumba nchini Kenya, Teresia Njenga, amesema maandamano hayo yamewaacha maelfu ya vijana wanaofanya kazi katika sekta hiyo bila kazi.

“Siku moja kama jana (Jumatano), wale vijana walikuja na kwenda nyumbani bila chochote kwa sababu wafanyabiashara walikaa mbali. Je, tunaweza kweli kuendeleza hili kila wiki?" Njega amehoji na kuongeza;

"Kwa kweli tunaiomba Serikali na upinzani kuona umuhimu wa kuwa na mazungumzo, maana watu wanateseka sana.”

Wafanyabiashara wa hoteli, ambao ndiyo kwanza wametoka kwenye janga la ugonjwa wa Uviko-19, ambapo biashara yao ilishuka na kupata hasra kwa kiasi kikubwa, sasa watrejeshwa huko ikiwa maadamano yataendele kwani, watalii na wageni wengine wanaweza kusitisha oda zao.

"Ninaweza kukuambia kufuatia kuibuka tena kwa maandamano sisi, kama sekta, sasa tunaona usitishwaji wa oda za wageni kama ambavyo iliwahi kutokea. Kwa kweli ni hali ya kusikitisha na inaturudisha nyuma,” amesema Mike Macharia, Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wamiliki Hoteli nchini Kenya.

Kwa upande wa wazalishaji wa bidhaa, wanayaona maandamano hayo kama kikwazo katika usafirishaji, lakini pia yanapunguza mahitaji ya bidhaa wanazozalisha, tena katika kipindi ambacho wanajaribu kupunguza mauzo kutokana na mfumuko wa bei.

Chama cha Wazalishaji wa Kenya (KAM) kilisema hasara ya kiuchumi kutokana na maandamano hayo itapunguza ajira, kwani kwa sasa wameendelea kulipa ushuru mkubwa na kuongezeka kwa gharama za uzalishaji kama vile mafuta na umeme.

"KAM inakubali kwamba raia wana uhuru wa kujieleza kwa amani, ni muhimu kwamba hili lifanywe bila kutatiza shughuli za biashara na kumlinda kila Mkenya," kimesema chama hicho katika taarifa yake na kuongeza;

“Usumbufu huo umekuwa na athari hasi kwa wazalishaji kutokana na hasara ya mauzo, usumbufu wa usafiri na usafirishaji na kuathiri wafanyakazi kupata sehemu zao za kazi na mnyororo wa ugavi wa wazalishaji pamoja na uharibifu na upotevu wa mali kama vile magari, ofisi, maduka, miundombinu na maduka.”

Nalo Shirikisho la Waajiri nchini humo (FKE) limewataka viongozi kuweka kipaumbele katika mazungumzo kwa kuwa maandamano hayo yanaharibu tija.

"Kutatizika mara kwa mara kwa shughuli za biashara na usafirishaji huru wa watu, bidhaa na huduma, sio jambo zuri kwa nchi. Isitoshe, tija ya wafanyakazi imeshuka kwa sababu ya wasiwasi na kutokuwa na hakika kunakotokana na maandamano," Afisa Mkuu Mtendaji wa FKE Jacqueline Mugo amesema.

Wadau wa siasa na uchumi wa nchi hiyo wanadhani kuwa maandamano hayo ni pigo maradufu kwa Rais William Ruto kwani yanakuja wakati ambapo Mahakama Kuu imesimamisha kwa muda utekelezwaji wa hatua mpya za ushuru katika Sheria ya Fedha, ikisubiri kuamuliwa kwa kesi hiyo.

Kwa upande mwingine Serikali ilikuwa na matumaini kwamba hatua hizo mpya za ushuru zingesaidia kupata mapato ya takriban Sh289 bilioni kama mapato ya ziada, na Waziri Mkuu Musalia Mudavadi amesema kwamba kila siku, ambapo kesi hiyo iko mahakamani, Serikali inapoteza takriban Sh650 milioni.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live