Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Maandamano ya kupinga utawala wa rais Ruto yaendelea Kenya

Maandamano Ya Kupinga Utawala Wa Rais Ruto Yaendelea Kenya.png Maandamano ya kupinga utawala wa rais Ruto yaendelea Kenya

Thu, 18 Jul 2024 Chanzo: Bbc

Polisi katika waliokuwa wakipiga doria katikati ya jiji la Nairobi nchini Kenya wametumia vitoa machozi kuwatawanya vijana waliokuwa wamekusanyika kwa maandamano dhidi ya serikali.

Kulikuwa na maafisa wengi wa polisi katikati ya jiji la Nairobi, ambalo limekuwa kitovu cha hatua ya awali ya maandamano ya vijana.

Jumanne ilikuwa siku nyingine ya maandamano makali huku shughuli za biashara zikisimama katikati ya mji huo pamoja na miji mingine kote nchini.

Wakati huohuo mtu mmoja amedaiwa kuuawa kwa kupigwa risasi eneo la Kitengela, Kaunti ya Kajiado wakati wa maandamano dhidi ya serikali huku wito wa kumtaka Rais William Ruto ajiuzulu ukiongezeka.

Kilichoanza kama maandamano ya amani katika mji wa Kitengela yaligeuka kuwa ghasia baada ya maafisa wa polisi kuwarushia vitoa machozi waandamanaji hao.

Hii ilisababisha makabiliano makali kati ya waandamanaji na maafisa wa kupambana na ghasia ambao walijibu kwa kuwarushia waandamanaji maji ili kutawanya umati.

Chanzo: Bbc