Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Maandamano tena Kenya licha ya serikali kuahidi kupunguza matumizi ya fedha

Maandamano Tena Kenya Licha Ya Serikali Kuahidi Kupunguza Matumizi Ya Fedha Maandamano tena Kenya licha ya serikali kuahidi kupunguza matumizi ya fedha

Tue, 2 Jul 2024 Chanzo: Bbc

Wanaharakati nchini Kenya wamewataka waandamanaji kujitokeza tena barabarani hii le Jumanne, huku wengi wakikataa ombi la Rais William Ruto la mazungumzo kufuatia uamuzi wake wa kuondoa mapendekezo ya nyongeza ya ushuru.

Takriban watu 24 waliuawa katika makabiliano kati ya waandamanaji na polisi wiki iliyopita, wakati bunge lilipovamiwa kwa muda mfupi na kuchomwa moto.

Maandamano hayo ambayo yameongozwa na vijana na kuandaliwa kwa kiasi kikubwa kwenye mitandao ya kijamii, awali yalichochewa na mswada wa fedha ulionuiwa kukusanya shilingi za Kenya bilioni 346 (dola bilioni 2.69) kupitia ushuru.

Lakini matakwa ya waandamanaji wengi yameongezeka katika muda wa wiki mbili zilizopita na kujumuisha wito wa kupambana na ufisadi na kumtaka Ruto ang'atuke, madarakani jambo ambalo linawasilisha mzozo mkubwa zaidi katika utawala wake wa miaka miwili.

Mahojiano ambayo Ruto aliyatoa Jumapili jioni ya runinga, ambapo alitetea zaidi vitendo vya polisi na serikali yake, yalionekana kuzidisha misimamo ya waandamanaji kurejea barabarani.

Siku ya Jumatatu, wanaharakati walikuwa wakishiriki vipeperushi kwenye mitandao ya kijamii ambavyo viliwataka watu kujitokeza katikati mwa jiji la Nairobi. Wengi walichapisha jumbe kupitia hashitagi ya #Occupy CBDD Tuesday.

Harakati za waandamanaji hazina uongozi rasmi, na haikufahamika ni kwa kiwango gani watu wangeitikia wito huu baada ya makumi ya maelfu kujitokeza wiki iliyopita katika baadhi ya maandamano makubwa zaidi nchini humo.

Katika majukwaa ya mitandao ya kijamii, wanaharakati wamekuwa wakijadili jinsi ya kudumisha kasi na shinikizo dhidi ya serikali baada ya kufaulu kuuzima mswada wa fedha

Chanzo: Bbc