Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Maandamano mengine yafanyika Morocco kuunga mkono Wapalestina

Gazaaaa Maandana Morocco Maandamano mengine yafanyika Morocco kuunga mkono Wapalestina

Mon, 26 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Maelfu ya wananchi wa Morocco wamefanya maandamano katika miji mbalimbali ya nchi hiyo kuwaunga mkono wananchi wa Palestina na kulaani jinai zinazoendelea kufanywa na jeshi la Israel huko Ghaza.

Mashirika mbalimbali ya habari yameripoti habari hiyo na kuongeza kuwa; Jumuiya ya Uungaji mkono wa Masuala ya Umma wa Kiislamu nchini Morocco imetangaza kuwa, maandamano 110 yamefanyika katika miji 50 ya nchi hiyo kwa ajili ya kuwaunga mkono wananchi wa Palestina.

Shirika la habari la Anadolu limenukuu taarifa illiyotolewa jana na jumuiya hiyo ikisisitiza kuwa, maandamano haya yalifanyika kote kote nchini Morocco siku ya Ijumaa.

Washiriki wa maandamano hayo walipiga nara za kulaani mauaji ya umati na jinai zinazofanywa na utawala pandikizi wa Israel dhidi ya raia wa Palestina na kuitaka jamii ya kimataifa kutekeleza wajibu wake wa kuokoa maisha ya raia. Maandamano ya Wamorocco ya kupinga uhusiano wa nchi yao na Israel

Taarifa hiyo imeongeza kuwa, waandamanaji nchini Morocco wamelaani ukatili wa utawala wa Kizayuni wa kuwatesa kwa njaa, kuwazingira kila upande na kujaribu kuwahamisha kwa nguvu watu wa Ukanda wa Ghaza.

Washiriki wa maandamano hayo wameishinikiza pia serikali ya Morocco kufuta makubaliano ya kuwa na uhusiano wa kawaida na utawala katili wa Israel.

Tetouan, Tangier, Meknes (Kaskazini), Agadir na Taroudant (Katikati) na Oujda (Mashariki) mwa nchi ni miongoni mwa miji ya Morocco kulikofanyika maandamano makubwa ya kuwaunga mkono Wapalestina siku ya Ijumaa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live