Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Maandamano mapya ya kupinga Rwanda mashariki mwa DRC

Polisiiiii Polisiiiii.png Maandamano mapya ya kupinga Rwanda mashariki mwa DRC

Fri, 16 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Maandamano mapya dhidi ya Rwanda na kukashifu "ushirikiano" wa jumuiya ya kimataifa na nchi hii inayotuhumiwa kuunga mkono waasi wa M23 yamefanyika siku ya Alhamisi katika miji miwili mikubwa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, waandishi wa habari kutoka shirika la habari la AFP wamebainisha.

Huko Bukavu, mji mkuu wa mkoa wa Kivu Kusini, mamia ya watu, wakisimamiwa na polisi, wameandamana kwa amani kudai ukombozi wa maeneo yamkoa jirani wa Kivu Kaskazini yanayokaliwa na M23.

Waasi wengi kutoka jamii ya Watutsi, M23 ("March 23 Movement"), wakiungwa mkono na vitengo vya jeshi la Rwanda, wamekuwa wakiendesha mashambulizi kwa zaidi ya miaka miwili huko Kivu Kaskazini, ambako mapigano yamezidi hivi karibuni karibu na mji mkuu wa mkoa wa Goma. "Muiachieni Bunagana iwe Huru! Muiachieni Rutshuru iwe huru! Muiachieni Masisi iwe huru!", wameimba waandamanaji waliokusanyika kwa mwito wa mashirika ya kiraia (mashirika, vyama, vyama vya wafanyakazi) huko Bukavu.

Ukombozi wa maeneo haya "utakuja hatua kwa hatua licha ya ahadi nyingi. Miaka inapita, vifo, mateso na kiwewe vinaongezeka katika sehemu hii ya nchi (..) Hili lazima likome sasa," amesema Adrien Zawadi, kiongozi wa ofisi ya uratibu wa mashirika ya kiraia.

"Ndugu viongozi, chukueni majukumu yenu katika kukabiliana na vita hivi vya uchokozi", imeandikwa kwenye mabango, wakati waandamanaji pia wakilaani "njama na unafiki wa jumuiya ya kimataifa ambayo inachochea na kujaribu kuzima moto katika kutumia vibaya uvumilivu na imani nzuri ya Wakongo."

Wametoa wito wa "kufungwa kwa mpaka na Rwanda" pamoja na Uganda, ambayo pia inashutumiwa kuwaunga mkono waasi, lakini pia "kuvunjika kwa uhusiano wa kidiplomasia" na baadhi ya mataifa ya Magharibi, hasa Marekani, Uingereza, Ufaransa. .

Katika mkoa wa mashariki wa Tshopo, huko Kisangani, wanaharakati wa vuguvugu la raia, wakiwa na vipaza sauti na kuvaa kitambaa chekundu vichwani mwao, pia wamemtaka Rais FĂ©lix Tshisekedi "kutangaza vita dhidi ya Rwanda" na "kuvunja uhusiano wa kidiplomasia" na nchi za Magharibi kwa sababu ya madai yao ya kuunga mkono Rwanda.

Kwa kusema "komesha vita Mashariki", mamia kadhaa ya wanawake waliandamana Jumatano katika mji mkuu Kinshasa, ambapo maandamano ya vijana kadhaa yalilenga vituo na balozi za Umoja wa Mataifa mwishoni mwa wiki iliyopita na Jumatatu na magari kuchomwa moto.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live