Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Maandamano makubwa yaripotiwa Afrika Kusini

C03C3D79 A695 4D7B 8C79 40F05F4E4F0E.jpeg Maandamano makubwa yaripotiwa Afrika Kusini

Sun, 12 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mji wa Cape Town nchini Afrika Kusini umeshuhudia maandamano makubwa zaidi kuwahi kufanyika katika jiji hilo katika miaka kadhaa ya karibuni wakati makumi ya maelfu ya watu wamekusanyika kutangaza mshikamano wao na Palestina, wakitaka kukomeshwa ukatili wa Israel huko Gaza.

Umati mkubwa wa watu uliandamana katikati mwa jiji la Cape Town siku ya Jumamosi, wakitoa wito wa kusitishwa vita vya mauaji ya kimbari vinavyoendelezwa na utawala haramu wa Israel katika Ukanda wa Gaza.

Yamekuwa moja ya maandamano makubwa zaidi kuwahi kushuhudiwa katika jiji hilo kwa miaka kadhaa, na yamkini yalishindwa kwa ukubwa na maandamano mengine kama hayo yaliyowahi kufanyika kupinga vita vya awali vya Israel dhidi ya Gaza.

Maandamano hayo yalianzia katika Msikiti wa Muir Street katika Wilaya ya Sita na kuishia katika bunge la mkoa wa Western Cape katika mtaa wa Wale.

Maandamano hayo, yaliyoandaliwa na mashirika kadhaa ya kiraia na vyama vya kisiasa, yanakuja zaidi ya mwezi mmoja baada ya utawala dhalimu wa Israel kufanya mashambulizi ya anga dhidi ya raia wa kawaida katika Ukanda wa Gaza, ambapo hadi sasa Wapalestina zaidi 11,000 wameuawa shahidi aghalabu wakiwa ni watoto na wanawake. Utawala wa Israel pia inatekeleza mzingiro wa kinyama wa pande zote dhidi ya Gaza.

Waandamanaji walijipanga katika mitaa ya Cape Town wakiwa na bendera na mabango yaliyoandikwa: "Kwa milioni, kwa bilioni, sisi sote ni Wapalestina" na "Kutoka Mto hadi Baharini, Palestina itakuwa huru."

Pia kulikuwa na nara zilizoelekezwa kwa Rais wa Marekani Joe Biden, kama vile "Je, umeua watoto wangapi leo?"

Maandamano ya wakazi wa Cape Town, Afrika Kusini kulaani jinai za utawala haramu wa Israel huko Gaza Mwanzoni mwa maandamano hayo, waandaaji walitoa wito wa nidhamu na kuwakumbusha hadhirina kwamba hawakuwa wanapinga Mayahudi, bali Wazayuni. Waandamanaji pia walipiga nara za kuunga mkono Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina, Hamas.

Taarifa kutoka Muungano wa Afrika Kusini wa Kususia Utawala wa Kizayuni wa Israel (BDS) siku ya Ijumaa ilisema kwamba watu huko Gaza wanakufa njaa kutokana na mzingiro mkali wa Wazayuni. Imetoa wito wa kusitishwa mara moja mapigano na kuwasilishwa kwa wingi misaada ya kibinadamu huko Gaza.

Padre Michael Weeder, Mkuu wa Kanisa Kuu la St George, ambaye aliwahutubia waandamanaji, ametoa wito kwa viongozi wa dunia kuacha kutumia fedha katika vita na badala yake waelekeze fedha zaidi katika kuleta amani. Mchungaji Allan Boesak, mwanaharakati mashuhuri wa kupinga ubaguzi wa rangi, ametoa wito kwa serikali ya Afrika Kusini kumtimua balozi wa utawala haramu wa Israel nchini humo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live