Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Maandamano makubwa yafanyika Niger

Maandamano Makubwa Yafanyika Niger Maandamano makubwa yafanyika Niger

Sat, 13 Apr 2024 Chanzo: Bbc

Idadi kubwa ya watu walijitokeza katika mji wa Yamai, mji mkuu wa Jamhuri ya Niger, wakitaka wanajeshi wa Marekani na nchi nyingine kuondoka nchini humo.

Niger tayari imefuta makubaliano ya kijeshi na Marekani mwezi uliopita, na hii inakuja miezi michache baada ya mamlaka ya kijeshi ya nchi hiyo kukata uhusiano kama huo na Ufaransa, ambapo hata vikosi vya utawala wake wa zamani wa kikoloni vilifukuzwa ambavyo awali vililetwa kupambana na wapiganaji wa jihadi katika eneo hilo kutoka nchi hiyo.

Nchi hiyo sasa imeikaribisha Urusi kwa msaada katika kupambana na wapiganaji wa jihadi.

Na siku ya Jumatano, wanajeshi wa kitaalamu kutoka Urusi waliwasili nchini humo kutoa mafunzo kwa wanajeshi wa nchi hiyo.

Chanzo: Bbc