Muungano wa upinzani nchini Kenya Azimio umesema kwamba unaendelea na maandamano dhidi ya serikali ya rais William Ruto kuanzia siku ya Jumatano hadi Ijumaa.
Akizungumza katika mkutano na vyombo vya habari naibu wa Muungano huo ambaye pia alikua mbunge wa Gichugu Martha Karua amesema kwamba harakati za Muungano huo kuishinikiza serikali kufutilia mbali muswada wa fedha hazitasita licha ya vitisho kutoka kwa seriikali.
Matamshi ya kiongozi huyo yanajiri siku moja tu baada ya baadhi ya vinara wa Muungano huo kupokonywa usalama kabla ya kufanyika kwa maandamano hayo siku ya Jumatano, Alhamisi na Ijumaa.
Hatahivyo Kinara wa Muungano huo wa Azimio Raila Odinga ambaye aliitisha maandamano hayo siku ya Ijumaa iliopita hakuweko wakat iwa mkutano huo.
Kulingana na Bi Martha Karua kiongozi huyo alikuwa akiangazia masuala muhimu zaidi wakati wa mkutano huo