Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Maandamano huku kanisa la Orthodox la Ethiopia likigawanyika

Maandamano Huku Kanisa La Orthodox La Ethiopia Likigawanyika Maandamano huku kanisa la Orthodox la Ethiopia likigawanyika

Mon, 6 Feb 2023 Chanzo: Voa

Wafuasi wa Kanisa la Othodoksi la Ethiopia wanaanza maandamano ya siku tatu siku ya Jumatatu huku mvutano na viongozi ukiendelea kuongezeka.

Takriban watu watatu waliuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa mwishoni mwa juma katika mji wa Shashemene, eneo la Oromia, baada ya vikosi vya usalama kufyatua risasi kanisani, kulingana na ripoti za vyombo vya habari vinavyohusishwa na kanisa hilo.

Mapigano yaliripotiwa katika maeneo mengine huko Oromia huku kanisa hilo likidai kukamatwa kwa wafuasi wake katika baadhi ya maeneo mkoani humo.

Wiki iliyopita, baraza kuu la kanisa hilo, sinodi, liliamuru waumini wake kuvaa nguo nyeusi kama ishara ya kuandamana wakati wa hafla ya Mfungo wa Ninawi ya kanisa kuanzia Jumatatu.

Ilijiri baada ya kanisa kushutumu serikali kwa kusaidia makasisi waliojitenga kutoka eneo la Oromia - ambao waliteua maaskofu bila sinodi kujua.

Makasisi waliojitenga walisema walikuwa na uungwaji mkono "mkubwa" huko Oromia.

Taarifa iliyotolewa na ofisi ya mawasiliano ya serikali ya shirikisho haikusema lolote kuhusu shutuma za kanisa hilo na matukio ya ghasia.

Lakini ilionya dhidi ya vikosi ambavyo havikutajwa jina ambavyo ilisema vimejaribu kusambaratisha nchi hiyo bila mafanikio na sasa vinafanya kazi ya kuzidisha tatizo hilo.

Mikutano ya hadhara ilifanyika katika jiji la Dessie, kaskazini mwa nchi, na nje ya nchi huko Washington DC.

Watu mashuhuri wengi wametoa taarifa zinazoonyesha mshikamano na kanisa huku wengine wakichapisha picha - kwenye mitandao ya kijamii - wakiwa wamevalia nguo nyeusi.

Chanzo: Voa