Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Maandamano Kenya: Watu watatu wafariki

Maandamano Kenya: Watu Watatu Wafariki Maandamano Kenya: Watu watatu wafariki

Thu, 20 Jul 2023 Chanzo: Bbc

Makumi ya watu wamelazwa hospitalini wakiwa na majeraha ya risasi huku takriban wengine watatu wakiripotiwa kufariki katika siku ya kwanza ya maandamano ya siku tatu nchini Kenya.

Matukio ya kutisha yalishuhudiwa katika siku ya kwanza ambapo polisi wameripotiwa kutumia risasi kukabiliana na waandamanaji wanaopinga kupanda kwa gharama ya maisha na wengine wengi kujeruhiwa.

Waangalizi wa haki za binadamu wamewalaani polisi kwa kile walichokitaja kuwa matumizi ya nguvu kupita kiasi.

Upinzani unasema siku ya kwanza ya maandamano imekuwa ya mafanikio na kuwataka wafuasi wao kujitokeza hii leo tena katika mji wa Nairobi.

Kwa upande mwingine, mamlaka zinasema kuwa ni mikoa michache tu iliyoathiriwa na kutangaza kufunguliwa kwa shule huko Nairobi na Mombasa.

Wakati wa maandamano kama hayo wiki jana, takriban watu kumi waliuawa kwa kupigwa risasi na polisi.

Makundi ya ndani, kimataifa na wanadiplomasia wa kigeni wameelezea wasiwasi wao mkubwa kuhusu hali nchini Kenya na kuzitaka pande zote mbili kutafuta suluhu kupitia mazungumzo.

Chanzo: Bbc